MWANDISHI wa Kitabu cha 'CHEO KIMEFUTWA' Laeticia Mukurasi amewaasa wanawake na wanavyuo Vikuu kuzijua sheria nchi, ajira, sera na miongozo ili waweze kujitetea pale unapotokea uonevu nafasi za ajira na katika jamii.


Hayo ameyasema leo Agosti 12, 2023 katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa sheria hizo zinaweza kutetea mtu pale anapopata madhira mbalimbali katika jamii na katika utendaji wa kazi.

Pia amewaasa kujiamini wanapofanya jambo lolote kwani umakini unaongezeka hasa mahali pa kazi au sehemu waliyoajiriwa pia katika ufanyaji kazi huo amewaomba kuhifadhi ya kile kitu wanachokifanya bila kujali ni wapi na lini kitatumika.

Laeticia amesema kuwa katika Ufanyaji wa jambo lolote amewaasa kujitambua na kutojichukulia poa wanapofanya jambo lolote maishani

Licha ya hayo pia amewaomba kufanya kazi kwa ubinadamu bila kujali mkubwa au mdogo kwa manufaa ya taasisi na jamii kwa Ujumla.

Mwandishi huyo ameeleza kuwa kama yeye asingekuwa jasiri, asingesoma sheria na miongozo mbalimbali ya serikali basi yeye asingerudi katika cheo chake ambacho kilifutwa ndani ya miaka mitatu.

Akielezea kitabu hicho ambacho toleo la kwanza alitoa mwaka 1995 na akiwa na harakati za mwanamke kupigania haki za ajira nchini Tanzania amesema historia na mambo aliyoyaandika katika kitabu hicho yaliyomtokea yeye mwenyewe asingekuwa na ujuzi wa sheria na kuwa na uthubutu basi haki yeke ingedhurumiwa na watu wachache.

Akisimulia jjnsi alivyoachishwa kazi Mwandishi huyo amesema alikuwa meneja pekee wa kike katika kampuni ya Fibreboards (Afrika) Limited kati ya mameneja saba na yeye peke yake ndiye aliyeondolewa kazini kwa misingi ya kupunguza matumizi ya ofisi huku mtu waliyekuja kumwajiri kufanya majukumu kama yake alikuwa akilipwa mshahara mkubwa kuliko mshahara wake.

Laeticia aliamua kupinga uamuzi huo kwa sababu alibaguliwa kijinsia pia uongozi wa kiwanda hicho ulikiuka taratibu za kumwachisha kazi.

Amesema katika kitabu hicho ambacho kimesheheni historia nzima ya harakati za mwanamke mmoja kupigania haki za ajira Tanzania amesema pia aliangalia mabadiliko ya sheria ya ajira na jinsi alivyoshughulikia mapungufu yaliyoainishwa katika toleo la kwanza la kitabu hicho.

Mwandishi wa Kitabu hicho pia ametoa rai kwa wanawake kumwonea huruma mwanamke mwingine pale anapopitia katika tabu shida na madhira mbalimbali sio kumsengenya na kumwona kama mtu asiyefaa.

Pia amewaasa kujua mazingira na njia tofauti tofauti za kutatua changamoto inayokukabili na sio kujichukulia sheria mkononi.

Kwa Uapnde wa wanufaika katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameonekana kuvutiwa na stori zinasimuliwa zimekuwa na manufaa kwao kwani masuala yanayozungumzwa yamekuwa yakigusa kila nyanja katika maisha.
Mwndishi wa Kitabu cha 'CHEO KIMEFUTWA' Laeticia Mukurasi, akizungumza na wananwake na wanavyuo katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023. 
Mwandishi wa Kitabu cha 'CHEO KIMEFUTWA' Laeticia Mukurasi, akizungumza na wananwake na wanavyuo katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati wa kumkaribisha Mwandishi wa Kitabu cha 'CHEO KIMEFUTWA' Laeticia Mukurasi na kufungua uwanja wa simulizi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023. 

Mmoja ya wafanyakazi wa TGNP akizungumza na wananwake na wanavyuo katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023. 




Baadhi ya Matukio mbalimbali katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...