Ndugu Soud Ayubu Chamshama wa Chang'ombe Maduka mawili jijini Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi Mzee Ayubu Salehe Chamshama (pichani), kilichotokea tarehe 11 Agosti 2023 nchini India alikokuwa kwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 15 Agosti 2023 kijijini kwao Kilole, Lushoto, Mkoani Tanga.

Kwa sasa Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe Maduka Mawili jijini Dar es salaam.

Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na marafiki popote pale walipo.

Enzi za uhai wake Marehemu Chamshama atakumbukwa kwa kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Tanzania Tea Blenders, vile vile alihudumu kwa muda mrefu kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC na pia alikuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
Marehemu Mzee Ayoub Salehe Chamshama


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...