Na: Calvin Gwabara – Morogoro. leo 11/08/2023
Kufuta kanuni bora za afya, Ufugaji bora wa mifugo, Uzalishaji bora wa mazao pamoja na uzalendo ni miongoni mwa mambo ambayo yakizingatiwa yanaweza kupunguza kama sio kumaliza kabisa janga kubwa la dunia la usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa nchini Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Prof. Robinson Mdegela mtaalamu wa Mgonjwa ya Wanyama na afya ya jamii ambaye ni mkuu wa Idara ya Tiba ya magonjwa ya wanyama na jamii yanayohusiana na Wanyama katika ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Mkoani Morogoro nchini Tanzania.
“Kidunia tuna janga kabwa la ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa na ni changamoto inayouwa watu kimyakimya na hii ni kutokana na takwimu kadhaa mfano ugonjwa wa Marelia unaua watu takribani 640,000 kwa mwaka,UKIMWI unaua watu karibu 840,000 wakati tatiz0 la usugu wa vimelea dhidi ya dawa linaua watu takribani 1,400,000 hii maana yake ni mara mbili zaidi ya watu wanaokufa kwa ugonjwa wa marelia kwa mwaka kwahiyo unaweza kuona ukubwa wa tatizo hili na linakua kila
mwaka” alifafanua Prof. Mdegela.
Prof. Mdegela amesema tatizo hilo linachangiwa na watu kula vyakula kama vile Kuku, Mayai, Nyama, Mbogamboga zenye mabaki ya dawa lakini pia tabia ya jamii kutumia madawa wanapoumwa bila kupima na kutomaliza dozi wanayopewa na hivyo inayofanya wadudu kufubaa badala
ya kufa.
“Dawa kama Tetesakline hatakiwi kutumia mtoto mdogo na akitumia inaharibu meno na mifupa lakini bahati mbaya sana chakula bora ndio hichohicho mayai,Nyama na maziwa na kwakuwa dawa hiyo pia wafugaji huitumia kuwapatia mifugo inapoumwa kama mfugaji hakuwa mzalendoa au mwaminifu unaweza jikuta unamlisha mtoto dawa kupitia vyakula hivo kwahiyo tunajitahidi kuwaelimisha wafugaji kitu gani kifanyike ili mazao yanayotoka yasiwe na dawa hizo kwasababi vikiwepo watu wanadhurika
kwa kupata dawa bila mhusika kuihitaji mwilini”. Aliezleza Prof.Mdegela.
Aliongeza “jambo la pili unapata dawa isiyo dozi kamili ambayo inasababisha kufubaa kwa vimelea vya magonjwa kwakuwa vinapata dawa ambayo ni ndogo vinaendelea kuwepo na vinatabia ya kutengeneza usugu kiasi kwamba hata siku ukiumwa ukapewa dawa hiyo huwezi kupona na ndio maana tunapata vifo vingi sasa hivi kwa mwaka kuliko marelia na nijanga la kidunia”.
Mtafiti huyo wa Mgonjwa ya Wanyama na afya ya jamiia ameendelea kusema kuwa muunganiko kati ya wanyama na binadamu ni mkubwa sana kwakuwa dawa zinazotumika kutibu magonjwa kwa wanyama ndizo hizohizo zinazotumika kutibu magonjwa ya binadamu akitolea mfano dawa streptomycin lakini ndio dawa inayowekwa kwa matumizi ya wagonjwa wa TB na hata salfa zinazotumiwa kwa wanyama wakiharisha ndizo pia zinatumika kwa binadamu.
Ameitaka jamii kuhakikisha wanagundua magonjwa mapema kwenda hospitali na kuzuia wanyama kuugua kwa kufuga kisasa lakini pia kuwapatia chanjo wanyama na ikitokea wameugua wafugaji wazingatie kunakuwa hakuna masalia ya dawa kwenye maziwa,nyama na mayai wanayowauzia watu kwa kuzingatia kipindi cha mpito cha kutotumia mazao hayo ya mifugo baada ya kuwapatia dawa.
“Sasa ndugu zangu hilo ndio tatizo kubwa sana mfano duniani nchi zilizoendelea huwezi kununua dawa au kutibu bila kufuata uratibu fulani na sisi bahti mbaya hicho kitu hatuna na mfugaji mnyama akaumwa na akamtibu hazingatii kipindi cha mpito kabla ya kuuza mazao ya wanyama wake maana kuna dawa unatakiwa usubirie siku tatu,tano,zingine saba hadi siku 14 kwahiyo utupe mayai siku 14, maziwa siku 14 au usimchinjen mnyama yoyote au kuku ndani ya siku hizo kama dawa inavyotaka tunaona
watu wanshindwa kwasababu ya uchumi mbaya”.Alieleza Prof. Mdegela.
Amesema hiyo inatokana na wafugaji wengi wakubwa na wadogo kuchukua mikopo bank na hivyo kushindwa kufuata kanuni za muda wa mpito kwa kutupa mazao hayo kwa siku zinazoelekezwa na kuwauzia watu wasiojua na kujikuta wanakula dawa zisizostahili.
”Lazima tufuate kanuni bora za ufugaji na inapotekea tatizo la kutibu na ikatokea hasara hiyo kwa nchi zilizoendelea huwarudishia gharama wafugaji kwakuwa wanakuwa wameikatia bima mifugo yao na imesajiliwa lakini tazama kwa nchi yetu watu waambiwa wakate bima zao kutibiwa hawataki mpaka Bunge linaweka sheria sasa kwa mifugo itakuwaje kwahiyo njia rahisi zaidi ni fugaji bora wa kuzingatia usafi wanyama wasiuge, pili tuchanje wanyama wetu na tatu inapolazimika tutibu laki ni tuzingatie
swala la muda wa mpito” alibainisha Prof. Mdegela.
Aidha amesema kuwa tatizo linagusa mazao ya kilimo kama mbogamboga kwakuwa nazo hupuliziwa madawa kuua wadudu na huchumwa bila kuzingatia muda wa mpito na kwenda kuuzwa na jamii kuzilla lakini pia baadhi hutumia mbolea toka kwenye mabanda ya kuku na mifugo ambayo imetibiwa na mbolea yake huwa na dawa na dawa ikiwekwa kwenye mbogamboga hizo mboga nazo hupata dawa na kumfikia bindmu.
Katika kukabiliana na Jnaga hilo kubwa Tanzania tayari imetengeneza mkakati mwaka 2023/2028 wa kupambana na usugu wa vimela vya magonjwa ambapo maabara za Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo nayo imechaguliwa katika kufuatilia na kuchunguza kama tatizo hilo linapungua au kuongezeka ambapo tayari maabara hiyo imetoa takwimu za masalia ya dawa,takwimu za ubora wa dawa na sasa wametoa takwimu zinazohusiana na viautilifu na kwa kushirikiana na wizara ya afya wametoa takwimu za
matumzi ya dawa asili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...