Na. WAF - Dar es Salaam

Serikali inatarajiwa kujenga Hospitali ya Wilaya ya Temeke katika eneo la Vikuruti lilipo Chamazi, Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ilikupunguza msongamano katika vituo vya Afya vilivyo ndani ya Temeke.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambapo amesema kuwa watu wamekuwa wakiongezeka hivyo vituo vya huduma vimezidiwa hali ambayo wanaonelea kupanua huduma kwa kuja na Hospitali hiyo.

“Rais Dkt. Samia amenielekeza niwaelekeze Hospitali ya Taifa Muhimbili - MUHAS kutoa ekari 30 kuipatia Manispaa ya Temeke pale Vikuruti ili kujengwa Hospitali nyingine ya Wilaya kubwa nzuri”, amesema Waziri Ummy

Amesema, Manipaa ya Temeke inaongezeko kubwa la watu takribani Milioni 1.6 lakini kukiwa na uhaba wa Vituo vya kutolea huduma hivyo tumeamua kama Serikali kujenga Hospitali ya Wilaya.

Hospitali hii ya Wilaya ya Temeke tutaijenga Vikuruti-Chamazi itasaidia zaidi kupunguza mzigo wa wananchi kufuata huduma maeneo ya hizi hospitali ya Temeke na Mbagala Rangi Tatu.’’ Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Awali akipokea taarifa juu ya huduma za Afya ndani ya Temeke, Waziri Ummy amewaomba watendaji wa Temeke kuhakikisha wanatafuta maeneo ilikuweza kujengwa vituo vya Afya.

“Mhe Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hashindwi, nyie tafuteni maeneo tutakaa sisi Wizara ya Afya na TAMISEMI kuona namna ya kupata maeneo ya kuweza kujenga hivi Vituo vya Afya ilikuweza pia kupata Vituo vya Afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...