Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea shada la maua alipowasili katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya AICC Balozi Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC wakimpokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili katika Ofisi zao jijini Arusha kuwatembelea.
Msimamizi wa Hospitali ya AICC akimueleza kitu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili katika Hospitali hiyo jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amembeba Mtoto wa kiume aliyezaliwa tarehe 09 Agosti 2023 katika Hospitali ya AICC alipotembelea hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Kituo cha AICC jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni kwenye Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimatifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jengo la AICC jijini Arusha alipozuru chumba hicho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea eneo ambalo kitajengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimatifa cha Mlima Kilimanjari (MKICC) alipotembelea Ofisi AICC jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea kituo hicho jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na watumishi wa AICC jijini Arusha alipotembelea Ofisi za kituo hicho jijini Arusha
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Mwakilishi wa Watumishi wa AICC Bi. Catherine Kilinda akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa AICC tayari kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akionesha zawadi aliyopewa na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza na watumishi wa AICC katika ofisi zao jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC jijini Arusha
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) atembelea ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha @AICCTZ kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo na kupanga kwa pamoja jinsi ya kutekeleza majukumu ya AICC kwa mwaka huu wa fedha.
Mhe Waziri katika ziara hiyo amezuru Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jingo la AICC , hospitali ya AICC, eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC) na kuzungumza na wajumbe wa bodi, menejimenti na watumishi wa AICC.
Akizungumza na watumishi hao Mhe. Dkt. Tax amewataka kuhakikisha huduma wanazotoa zinaendana na mahitaji ya wakati uliopo ili kuhimili ushindani wa soko la biashara ya utalii wa mikutano na kuiwezesha taasisi yao kupata mikutano mingi zaidi.
Mhe. Waziri pia amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuitangaza nchi pale wanapotokea kuandaa mikutano ya Kimataifa kama ilivyotokea kwa mkutano uliofanyika nchini hivi karibuni wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliojadili rasilimali watu.
Katika ziara hiyo Dkt. Tax aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bw. Ephraim Mafuru.
Mhe. Dkt. Tax amefanya ziara ya siku moja ya kutembelea AICC kwa ajili ya kujadiliana nao na kuona ni jinsi gani wanaendana na mikakatiitakyoiwezesha AICC kuendelea kuwa Kituo bora cha Mkitano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Ziara hii ni ya kwanza kwa Mhe Waziri tangu ateuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwezi Oktoba 2022.
Kituo cha AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Taasisi nyingine ni Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam (CFR) pamoja na Mpango wa Hiari wa Kujitathmini wa Afrika (APRM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...