Na. Josephine Majura, WF, Dar es Salaam
Serikali imewaalika wadau wa Sekta Binafsi kutoka Uingereza kuwekeza nchini ili kusaidia juhudi za Serikali kufikia malengo yake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey.
Mhe. Chande alisema Serikali imekamilisha utiaji saini na UK Export Finance kwenye Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na kuendeleza barabara ya Tunguu - Makunduchi -kilomita 28, Fumba - Kisauni-Mazizini -kilomita 13.2, na mkoani - Chake Chake and Pemba Airport kwa ukubwa wa kilomita 43.5
.
Katika kikao hicho Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Chande aliwakaribisha Wawekezaji mbalimbali kutoka Uingereza kuja kuwekeza katika sekta za uzalishaji, uongezaji thamani na utalii nchini Tanzania.
“Nakukaribisha wewe na wafanyabiashara na wawekezaji wa kiingereza kuleta mitaji yenu Tanzania ” alisema Chande.
Kwa upande wake Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey Humphrey, alisema watashirikiana na Serikali kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika na kuendekeza kuwekeza katika vipaumbele vya kibiashara vilivyopo nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Worldline kutoka Ufaransa, Bi. Caroline Jesequel, inayojihusisha na masuala ya utengenezaji wa mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, ambae yupo nchini nchini na ujumbe wake kujifunza na kuona mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa njia ya mtandao katika Sekta ya Benki na kwenye Taasisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...