Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa baraka kwa wanafunzi 30 wanaosoma Taasisi ya Teknolojua Dar es Salaam( DIT) wanaochukua digrii ya kwanza ya Uhandisi na sasa wamepata nafasi ya kwenda kusoma nchini China.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaaga wanafunzi hao wa DIT ambao wanakwenda kusoma katika
Taasisi ya Chongqing (CQVIE) ya nchini China Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda amewahimiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii.
Wanafunzi hao wamepata nafasi ya kwenda kusoma nchini China ni kutokana na makubaliano ya ushirikiano DIT na Taasisi ya Chongqing (CQVIE) ambapo Waziri Mkenda anasema anatamani vijana wengi wapate nafasi ya kusoma kwenye taasisi hiyo.
Profesa Mkenda ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wanafunzi hao watakapokuwa China wahakikishe wanasoma kwa bidii na kutambua kwamba taifa lao linawategemea na ujuzi watakaoupata utakuwa na tija kwa nchi.
"Wanafunzi ambao mnakwenda huko China, nendeni mkasome kwa bidii mpate maarifa ambayo yatakuja kulisaidia taifa, hivyo mkiwa huko iwakilisheni nchi vizuri, mkae mfano wa kuigwa."
Aidha amesema hatua hiyo ya wanafunzi wa DIT kupata nafasi ya kwenda kusoma pia inatokana na ni matunda ya mageuzi yaliyofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya elimu kupitia ziara zake nje ya nchi kupanua wigo wa ushirikiano katika sekta hiyo.
Pamoja na hatua hiyo Waziri Mkenda amesema mazungumzo yanaendelea kati ya serikali ya China na Tanzania lengo ni kuona zinapatikana fursa nyingi zaidi ya kielemu hususani kwa DIT na kuweza kusafirisha wanafunzi zaidi ya 300 kuwatakaokwenda kusoma China na wafanyakazi wa chuo hicho kwenda kujengewa uwezo ncini humo.
Amesema awali wameshuhudia mabalozi wa nchi hizo mbili wanasaini makubaliano ambayo sasa utekelezaji wake umefikia na wameanza na wanafunzi hao 30 ambao wanakwenda kusoma nchini kwa miaka miwili na baada ya hapo watarudi kuendelea na masomo yao DIT kumalizia mwaka uliobakia wa masomo.
Akifafanua zaidi kuhusu wanafunzi hao Profesa Mkenda amesema wananfunzi hao wamepata nafasi ya kusoma masomo yao ya uhandisi kwa mwaka mmoja chuo cha DIT miaka miwili ya Stashahada watasoma China na kurudi kumalizia miaka miwili ya shahada ya kwanza.
Awali Mkuu wa Chuo cha DIT, Profesa Preksedis Ndomba ameeleza kwamba tukio hilo ni kubwa na la kihistoria la kuwaaga wanafunzi 30 wanaosoma Uhandisi Ujenzi ambapo kwa chuo na sasa wanakwenda China kusoma.
Amesema wanafunzi hao wakiwa China watapa muda wa kusoma kwa vitendo zaidi na hiyo itawawezesha kuwa watalaam wazuri baada ya kuhitimu masomo huku akitumia mafasi kueleza DIT mitaala yake inakubalika katika nchi nyingi ikiwemo China.
Kuhusu sifa ambazo zimetumika kuwapata wanafunzi hao amesema sifa kubwa ni uwezo wao wa kufanya vizuri katika masomo na kufauli vizuri lakini sifa ya pili ilikuwa ni utayari wa waanafunzi."Baada ya kupata majina yao kutokana na kufaulu vizuri tulianza kuuliza kama wapo tayari.
"Wapo wanafunzi wamefaulu vizuri lakini hawakuwa utayari lakini wengine wao mbali ya kufaulu wamekubali kwenda kusoma China na programu hii itakuwa ya miaka mitano kuanzia mwaka huu, wanafunzi wetu wanakwenda na wao wanakuja kwetu, ni programu ya kubadilishana wanafunzi."
Sehemu ya wanafunzi wa DIT ambao wamepata nafasi ya kwenda kusoma nchini China ambako wakiwa huko watasoma mwaka wa pili na watatu na kisha kuja kumalizia mwaka wa nne DIT
Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Che Zhao Guang akizungumza kuhusu ushirikiano baina ya taasisi hizo katika kutoa elimu na hasa inayohusu masuala ya uhandisi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi wa DIT wanaokwenda masomoni nchini China
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...