Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, (wa pili kulia) akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amemwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano huo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia), akishiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk (wa pili kushoto), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Balozi Kennedy Gaston (kushoto), baada ya Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Luanda, Angola

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...