*Wateja kukopeshwa bila ya riba.
KAMPUNI ya simu za mkononi Infinix Mobile Tanzania inawajuza wateja wa simu za mkononi kuwa ule Mwezi wa Infinix ndio huu na tayari pirika pirika za kuupamba Mwezi huu zimeshaanza na ili kuwafikia wateja wake kwa ukaribu zaidi Infinix imezindua promosheni ya JIPATE NA INFINIX ambayo itakuwa ikiendelea katika maduka yote ya simu nchini kote.

“Promosheni ya JIPATE NA INFINIX ni ya kipindi cha Mwezi mzima katika maduka yote ya simu nchini kote ndani ya msimu huu ukinunua simu hizi za Infinix, Note 30, Note 30 pro, Note 30 vip, Zero ultra, Hot 30, Hot 30i, Hot 30 Play au Smart 7 utajiweka kwenye nafasi kupata Jokofu, pikipiki, Laptop na zawadi nyingine nyingi”, aliyasema hayo Msanii wa kizazi kipya Frida Amani ambaye ndio balozi wa promosheni hii.

Balozi wa Jipate na Infinix Frida Amani akizungumza na wateja siku ya uzinduzi
Aliongeza, nimekuwa mwanafamilia wa Infinix kwa muda mrefu tangu kipindi cha Infinix HOT 10T na hadi sasa nimekuwa nikivutiwa sana na simu za kampuni hii kikubwa kinachotofautisha simu za Infinix na zingine ni uhimili wa simu kukaa na chaji kwa muda mrefu simu za Infinix zipo imara sana ili kuthibitisha hili nunua Infinix mkoa wowote uliopo na jambo jema zaidi ukihitaji huduma ya kukopa ipo kwa simu zote za Infinix na Riba imeondolewa kabisa kwa Infinix NOTE 30”.

Infinix Note 30 ilizinduliwa rasmi nchini Tanzania Mwezi wa sita mwaka huu ni simu yenye sifa nyingi sana na sifa kubwa ikiwa ni ya fast chaji ya watt 33 inauwezo mkubwa wa kupitisha nishart kwenda kwenye battery na kwa muda wa dakika 30 inakupa asilimia 70% ya chaji.

Kwa maelezo zaidi tembelea @infinixmobiletz au wapigie 0659987284.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...