Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mheshimiwa Joko Widodo amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku mbili kuanzia tarehe 21 – 22 Agosti, 2023.
Ni majira ya saa 10:40 alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb).
Viongozi wengine walioshiriki mapokezi ya Mheshimiwa Widodo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele, Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo Jatmiko pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mheshimiwa Joko Widodo akipokelewa na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku mbili Tarehe 21 - 22 Agosti, 2023. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...