LUDEWA,NJOMBE

Wakazi wa kijiji cha Ilininda wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, wameamua kuchangishana fedha ili kuanza ujenzi na ununuzi wa vifaa vya maabara ya kijiji,itakayosaidia upatikanaji wa vipimo vya magonjwa ya binadamu,ili kuepukana na ramli chonganishi ambazo zimekuwa chanzo cha migogoro na mauaji.

Wananchi wa kijiji hicho akiwemo Exavel Mlelwa,Teodosya Msanga na Ditrick Mlelwa wanasema kukosekana kwa huduma ya upatikanaji wa vipimo katika ngazi ya vijiji ni mojawapo cha kukithiri kwa imani za kishirikina ikiwemo ramli chonganishi,kutokana na watu kutumia dawa bila kupima na kubaini aina ya ugonjwa unaomsumbua.

"Tumekuwa tukipata shida sana magonjwa yanapojitokeza na manesi wetu wanafanya kazi kwa kukisia tu sasa ile ni changamoto na wakati mwingine tumekula hadi madawa sio sahihi kutoakana na homa uliyokuwa nayo kwa hiyo kwa jambo hili tunaona kwetu ni zuri sana"amesema Mlelwa

Kutokana na changamoto hiyo,wakazi wa kijiji hicho akiwemo Johson Mgimba wameamua kushikana mkono na kuchangishana fedha, kwa kushirikiana na wadau wa wengine wa afya ili kuanza rasmi ujenzi wa maabara zoezi ambalo litajumuisha na ununuzi wa vifaa.

"Hili ni wazo ambalo tuliibua kwa kuona kuna uhitaji huo na kuamaua kupambana na hatimaye leo tumefikia kiasi hiki cha mchango wa milioni tano na laki saba na tulivyomaliza kufunga hesabu kunamwananchi mwingine katoa kwa hiyo leo tumefanya uzinduzi kwa shilingi milioni sita na laki mbili"amesema Mgimba

Changamoto ya Matumizi ya dawa bila vipimo imetajwa kuwa sababu ya kuchochea Ramli chonganishi, kutokana na wakazi hawa kwenda kutafuta chanzo cha magonjwa yanayowasumbua, licha ya kwamba hali imezidi kuwa mbaya kila uchwao.

Hata hivyo wameiomba serikali kuwashika mkono ili kuongeza nguvu pale watakapoishia ili kukamilisha ujenzi wa maabara na ununuzi wa vifaa tiba.
"Tunaiomba serikali ituunge mkono kwenye hili ili itutafutie baadhi ya vifaa ambavyo sisi tutashindwa kwasababu kuna vifaa vingine huwa na gharama kubwa"amesema Lawi Mnyanga.


Kupatikana kwa maabara kwaajili ya huduma za vipimo vya magonjwa ya binadamu katika ngazi ya vijiji kunatajwa kuwa huenda ikawa njia moja wapo ya kupunguza ramli chonganishi katika maeneo hayo sambamba na kupunguza mauaji yanayotokana na imani za kishirikina.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...