Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), Profesa Ibrahim Lipumba leo Agosti 23, 2023 jijini Dar es Salaam wamezindua mpango wa kukuza mjadala ya vyama vingi na kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika siasa na uchaguzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza mara baada ya kuzindua mpango wa kukuza mjadala ya vyama vingi na kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika siasa na uchaguzi leo Agosti 23, 2023 jijini Dar es Salaam wamezindu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 23, 2023 amezindua mpango wa kukuza mjadala Wa vyama vingi na kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika siasa na uchaguzi.
Uzinduzi huo umefanyika kufuatia Mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) uliojadilli hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Katika ushiriki wake, Rais Mwinyi akizungumza kuhusu hali ya demokrsia, amesema mchakato wa mabadiliko ya sheria yaliyofanyika pia ameongelea suala la vyama vingi na namna ambayo demokrasia ya vyama vingi ilivyolindwa nchini.
Licha ya hayo ametoa wito kwa TCD kuendeleza kuandaa mikutano mingine ili kuendeleza demokrasia kwa kuwa inaonesha ukomavu wa kisiasa nchini.
Pia Rais Mwinyi amesema mapendekezo ya wadau yaliyotolewa katika mkutano huo yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kurejea mchakato wa katiba mpya, kubadili sheria za uchaguzi na kuwa na usimamizi mmoja kwa chaguzi zote.
Awali wakizungumza kuhusu nini kifanyike ili kuboresha Uchaguzi ujao(2024/25) na ziwe huru na haki, Mwanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ihusishe Chaguzi zote za serikali za mtaa na uchaguzi mkuu.
Ili uchaguzi uwe huru na haki inabidi mageuzi makubwa kwenye sheria zinazosimamia uchaguzi. Hata hivyo kumekuwa na mkwamo kwenye mchakato wa kupata katiba mpya. Hadi sasa hakuna hatua iliyotekelezwa ya kuwa na katiba mpya, hadi sasa hakuna kamati ya wataalamu ili kuanisha katiba ya sasa na rasimu ya Warioba ili kuja na kinachotakiwa.
Inawezekana mchakato wa katiba ukawa mrefu, lakini tunaweza kuwa na sheria mpya ya uchaguzi. Inawezekana katiba ikasema Rais wa JMT atateua wajumbe wasiozidi saba wa uchaguzi, lakini katiba haijasema atateuaje, kwa hivyo sheria ya uchaguzi itasema kuhusu Rais atateuaje bila kuvunja utaratibu. Kwamba mchakato wa jopo utakuwa wa watu kuomba na kutakuwa na usaili na kisha rais kuteua. Inachotakiwa ni wadau kukubaliana. Hii itafanya kusiwe na haja ya tume huru na uchaguzi.
"Tukiendelea kuwa na mkwamo wa hoja tutakaa hadi 2025 na hakutakuwa na katiba mpya."
Pia amesema Sheria ya uchaguzi inabidi iseme maafisa wengine wa uchaguzi watakavyopatikana na suala la idara ya TAMISEMI kuendesha uchaguzi wa serikali za mtaa uondolewe.
Kwa upande wa mzungumzaji wa pili kutoka NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amesema kuwa Kilichofanyika 2019 na 2020 sio uchaguzi, suala hilo halina ubishani mkubwa akizungumzia nini kifanyike ili kufanikisha uchaguzi wa 2024 na 2025 amesema NCCR-Mageuzi wanasita kusema nini kifanyike, kwa kuwa rejea hazioneshi kama kumewahi kufanyika uchaguzi.
"Pia hatuwezi kuzuia 2024/25 isije, hatuwezi kuzuia kilichofanyika 2019/20 kutofanyika 2024/25. Lakini tunatamani mwaka 2024/25 kufanyike uchaguzi." Amesema
Na mzunguzaji kutoka CHADEMA, Reginald Munisi amesema kuwa kuwe na chombo kitachokuwa kinafanya rejea cha kufanya baada ya uchaguzi, chombo hicho kiundwe na taasisi zisizo za kiserikali, Viongozi wa dini na viongozi wa serikali.
Pia amependekeza kama kutakuwa na kura za maoni kuwe na chombo huru cha kusimamia kura za maoni, au tubadili katiba.
Mzungumzaji kutokaChama Cha Mapinduzi (CCM) Anamringi Macha anesema kuwa hakubaliani na swali la nini kifanyike kama hakuna kitu kimefanyika kwahiyo ni muhimu tujadili nini kiendelee kufanyika.
Amesema kwenye mchakato wa katiba kuna mkwamo kwa kuwa hatukuridhiana, kuna wengine walisema kuna watu wamekuja na katiba yao mfukoni, Mchakato wa katiba ni tofauti na kitabu cha hadithi hivyo utachukua muda.
Pia amesema kuwa anakubaliana kufanya mabadiliko ya katiba ili kukidhi mahitaji ya uchaguzi, hata hivyo baadhi ya hayo tayari yamefanyika kama kuondoa zuio la kufanya mikutano ya vyama vya siasa.
Pia amekili kuwa utashi wa kisiasa upo lakini kinachotakiwa kutolewa kwa elimu ya uraia na kuwa elimu hiyo haina mwisho hivyo kunakuwa na umuhimu wa watu kuelimishwa kuhusu utashi wa kisiasa.
Mzungumzaji ambaye pia ni mlezi wa vyama vya siasa kutoka kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa , Sisti Nyahoza amesema kuwa amesema kuw achangamoto zipo ndani nje ya vyama na zinatokana na maneno wanayosema hao wanaoshiriki uchaguzi.
Pia ametaja changamoto nne ambazo ni Uelewa wa demokrasia na kuamini demokrasia, Sheria Utendaji na Rushwa hizo ndio sababu zinafanya tusiwe na uchaguzi wa huru na haki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...