Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila, Agosti 17,2023 amevunja uongozi wa Soko la Mabibo na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU} kufanya uchunguzi wa kina katika soko hilo na watakao bainika hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
RC Chalamila ametoa kauli hiyo alipofika katika soko hilo kutatua mgogoro baina ya wafanyabishara biashara wasiowaaminifu wakiongozwa na Uongozi wa Soko hilo na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Aidha RC Chalamila amekemea watu wachache, wabinafsi, katika soko hilo kukwamisha jitihada za serikali na kamwe wasijaribu hata kidogo masoko lazima yaboreshwe Serikali ikusanye mapato yake na wafanyabishara wafanye biashara zao sehemu rafiki.
"Hatuwezi kuacha watu wachache wanajinufaishe na Serikali inakosa mapato, Mkurugenzi wa Manispaa anza kazi leo," Alisema Chalamila
Hata hivyo RC Chalamila amebainisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan dhamira yake ni kuboresha masoko,na kwamba tayari kiasi cha shilingi milioni 600/= kimetengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya kuanza kazi ya kuboresha Soko hilo.
Vilevile Mkuu wa Mkoa amesema uongozi uliokuwepo ulikuwa ukikusanya fedha nyingi lakini zilikuwa zikiishia katika matumbo ya watu wachache badala ya kuwanufaisha walio wengi,ambalo alikiri wazi kutokubaliana nalo.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hashim Komba ameweka bayana Changamoto zilizoko katika Soko hilo na kuonyesha dhamira ya Wilaya yake kutaka maboresho ya Soko hilo muhimu kwa masilahi mapana ya Umma ambapo amesema ni kweli mmiliki halali wa soko hilo ni Urafiki wameshaketi na kukubaliana Soko hilo kuendeshwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo hivyo tayari Manispaa imeshatenga shilingi millioni 600 ili kuanza Ukarabati wa Soko hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...