Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa kilimanjaro Nurdin Babu ametoa wiki mbili kwa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanasimamia hatua za mwisho (finishing) kukamilika kwa haraka jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Maabara na nyumba ya mtumishi katika zahanat ya Naibili
Ameyasema hayo akiwa kwenye ziara wilayani Siha mkoani Kilimanjaro akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita chini Rais Dk.Samiha Suluhu Hassani
Amefafanua Rais Samia ametoa fedha Sh. 271,096,536.00 lengo wananchi wake wapate huduma za afya kwa wakati."Sipo tayari kuona ujenzi huo, kamati ya usimamizi unasuasu, hivyo naagiza kituo hicho kijegwe usiku na mchana, "amesema Babu.
Mbali na hayo yote Mkuu wa Mkoa amewataka kila kiongozi kwa nafasi yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha kujua kila mradi unaotekelezwa katika sekta yake na kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha mradi unamalizika ukiwa na viwango vya hali ya juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...