Na Nasra Ismail, Geita
SHULEya msingi Kasungamile iliyopo katika kata ya Nyakamwaga Halmashauri ya wilaya ya Geita inakabiriwa na uhaba mkubwa wa walimu pamoja na uchakavu wa madarasa Hali inayopelekea wanafunzi kusoma katika mazingira magumu ambayo si rafiki kupata elimu.

Akibainisha hayo mwalimu mkuu msaidizi katika shule hiyo Monko k Charles alisema shule hiyo inajumla ya walimu 7 TU ukilinganisha na wanafunzi ambapo shule Ina jumla ya wanafunzi 603 hali inayokwamisha ufaulu na maendeleo ya elimu katika shule hiyo.

Mapungufu hayo yameibuliwa baada ya kamati ya siasa ya chama Cha mapinduzi (CCM)kata ya Nyakamwaga ilipoenda kutembelea shule hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Mahuma Juma Nzagabulu inayoendelea kufanya ziara katika kata zote za Nyakamwaga Kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Baada ya kufanya ukaguzi katika shule hiyo Kamati hiyo pia imebaini uchakavu mkubwa wa miundombinu ya madarasa Hali inayopelekea wanafunzi kusomea katika mazinngira hatari Kwa afya zao.

Kwa upande wao wananchi na wanafunzi waliiomba serikali kuitazama shule hiyo Kwa jicho la tatu kwani mi shule pekee ambayo inapatika katika maendeo hayo na inapokea wanafunzi wengi zaidi ikilinganishwa na idadi ya walimu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...