Njombe
Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imesema kupitia maboresho makubwa yanayokwenda kufanyika kwenye uwanja wa michezo wa Benjamini Mkapa maarufu kwa Mkapa,serikali inakwenda pia kuweka mfumo wa internet bure ili kuwawezesha mashabiki kupata huduma hiyo ndani ya uwanja.
Katibu mkuu wa wizara hiyo Saidi Yakubu amebainisha hayo mkoani Njombe wakati akifungua kikao kazi cha 14 kwa maafisa maendeleo utamaduni na maafisa maendeleo ya michezo wa mikoa yote ya Tanzania bara kilichofanyika mjini Njombe.
"Tunakwenda kushirikiana na wenzetu wa wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari watatuwekea mfumo wa WiFi pale bure utakuwa ukiingia uwanjani kuangalia mpira lakini pia utakuwa unapata free WiFi itakuwepo pale"amesema Yakubu.
Katika mkutano huo katibu amegawa mipira hamsini na minne kila mkoa ambapo mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayai amesema mipira hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Samia Taifa CUP yatakayofanyika Oktoba mwaka 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...