MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba Serikali ipo katika hatua ya mwisho ya kuanza utekelezaji wa mpango wa wake wa mageuzi makubwa  katika sekta ya elimu ambao unaohitaji ushiriki na jitihada za pamoja kutoka kwa wadau na wahisani mbali mbali  wa maendeleo katika kufanikisha vyema utekelezaji huo.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Ofisini Kwake Migombani Mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungunza na Mwakilishi Mkaazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulia Maendeleo ya Watoto  (UNISEF), Bibi Elke Wisch.

Amefahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana jihitihada za ushirikiano  wa shirika hilo la UNISEF katika kuendeleza ushirikiano katika sekta ya Elimu hasa kwenye  hatua za maandalizi ya watoto katika kupata elimu bora.

Hata hivyo, Mhe. Othaman amesema kwamba  shirika hilo limekuwa na mchango mkubwa  katika maeneo mbali mbali yanayohusu elimu, usafi wa mji na hata katika  masuala ya mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi jambo ambalo linaisaidia Zanzibar kupiga hatua kwenye jitihada za kuendeleza mapambano yake kwenye maeneo hayo .

Aidha Mhe. Othman ameliomba shirika la UNISEF kuangalia uwezekano wa kusaidia masuala ya Lishe kwa watoto wadogo maskulini ili kuepuka watoto kula vyakula vinavyotoka  viwandani ambavyo huwekwa sukari nyingi jambo lenye  uwezekano wa kuwepo athari kubwa kwa watoto.

Aidha ameitaka jamii kubadili mfumo wa maisha ikiwemo kuepuka kuwazowesha wato kula vyakula vyenye sukari kwa wingi ili kuepusha madhara ya kula vyakula vya namna hiyo.

Kwa upande mwengine Mhe. Othman amesema kwamba Zanzibar inaendelea kuathrikana na changamoto za tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ambapo maeneo kadhaa Unguja na Pemba yanaendelea kuathiriwa na tatizo hilo licha ya kuwepo jitihada mbali mbali za serikali na wadau katika mapambano dhidi ya changamoto hiyo.

Ameongeza kwamba katika kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu kuwepo kwa mikakati makhusi itakayosaidia kupunguza athari zinazotokana na hali hiyo.

Amefahamisha kwamba kutokana na changamoto hiyo, Zanzibar hivi karibuni  pia  itazindua utekelezaji wa mpango wake wa kitaifa wa kurithisha Zanzibar kuwa ya kijani na kuiyomba Unisef kuwa tayari kusaidia jambo hilo  muhimu litakalochangia sana kupunguza athari zinazotokana  na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Mwakili huyo makaazi wa Unisef Kanda ya Afrika Mashariki Bibi Elke Wisch,ameahidi kwamba shirika hilo litaendelea kuisaidia Zanzibar katika maeneo mbali mbali hasa kuandaa mazingira ya elimu bora kwa watoto ikiwa ni jitihada za kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar.

Ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika jitihada zake mbali mbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi , ukimwi na usafi wa mji Sambamba na Shirika hilo kuangalia na kuzingatia maeneo mengine mapya yanayoweza kutekelezwa kati ya shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...