MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP), umesema kuwa Mafunzo yaliyotolewa yatawasaidia na yamewajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, leo Agosti 11, 2023 jijini Dar Es Salaam, Mtendaji kutoka Idara ya Mafunzo na Ujengaji Uwezo wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai amesema Wawakilishi wa asasi za kiraia zilizo katika mitandao yote ya TGNP ikiwa ni pamoja na wanavituo vya taarifa na maarifa na wanaharakati wengine ngazi ya Jamii wanepikika vizuri hivyo kazi waliyonayo ni kwenda kuyafanyia kazi yale waliyoelimishwa kwa siku tano.
"Mafunzo haya yatatuwezesha kuwa na nyenzo kwaajili ya kutetea na kuangalia mapungufu yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za kijamii na mahala pa kazi." Amesema Anna
Amesema mafunzo hayo pia yamewajengea uwezo wa kutengeneza mwongozo na mbinu bora za ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii kwa mtizamo wa kijinsia pia kutengeneza mikakati ya namna ya kuwa na mifumo thabiti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamiii katika mtizamo wa kijinsia ili kuimarisha taasisi zenye mifumo bora ya kuhakikisha kuna ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii hususani utoaji wa huduma.
Akizungumzia kuhusiana na TGNP, Anna amesema mtandao huo unawategemea wawakilishi wa Asasi za kiraia kuwawakilisha vyema kwani hawana matawi katika mikoa na wilaya.
Amesema wawakilishi hao watabeba agenda za TGNP kuhamasisha masuala ya kijinsia, elimu, afya na kufuatilia bajeti yenye mrengo wa jinsia kwani ni muhimu na kuhakikisha yale wanayoyapigania yanafanyiwa kazi, kutengewa bajeti lakini pia kutumika kama ilivyokusudiwa.
Mtendaji kutoka Idara ya Mafunzo na Ujengaji Uwezo wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano kwa wawakilishi wa Asasi za kiraia za wilaya mbalimbali zilizochaguliwa kupata mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Nemes Mabung’ai akikagua kazi za vikundi za wawakilishi wa Asasi za wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali jijini Dar es Salaam leo hayo leo Agosti 11, 2023.Mwezeshaji, Nemes Mabung’ai akizungumza na wawakilishi wa Asasi za wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali jijini Dar es Salaam leo hayo leo Agosti 11, 2023.
Mmoja wa wawakilishi wa Asasi za kiraia akitoa shukrani mara baada ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali jijini Dar es Salaam leo hayo leo Agosti 11, 2023.
Matukio mbalimbali katika mafunzo ya wiki nzima.
Picha ya Pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...