Na Nasra Ismail, Geita

SHULE ya Msingi Kasungamile iliyopo Kata ya Nyakamwaga Halmashauri ya Wilaya ya Geita inakabiliwa na changamoto ya  uhaba wa walimu pamoja na uchakavu wa madarasa.

Hali hiyo imeelezwa kusababisha  wanafunzi kusoma katika mazingira magumu ambayo si rafiki kupata elimu.

Hayo yameelezwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Monko  Charles wakati Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) ya Kata hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mahuma Nzagabulu kufanya ziara ya kutembelea shule hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani.

Hivyo Mwalimu  Charles ameiambia Kamati ya Siasa ya Kata kwamba kwa sasa  shule hiyo inajumla ya walimu saba tu  wakati wanafunzi waliopo ni 603,  hali hiyo imedai inakwamisha ufaulu na maendeleo  ya elimu katika shule hiyo.

Hata hivyo Kamati ya Siasa ya Kata kufanya kufanya ukaguzi katika shule hiyo pia imebaini uchakavu mkubwa wa miundombinu ya madarasa hali inayosababisha  wanafunzi kusomea katika mazinngira hatari kwa afya zao.

Kwa upande wao wananchi na wanafunzi wameiomba Serikali kuitazama shule hiyo Kwa jicho la tatu kwani ndio shule pekee  inayopatika maendeo hayo na inapokea wanafunzi wengi zaidi ikilinganishwa na idadi ya walimu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...