Na.Mwandishi Wetu_DODOMA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Adolf Mkenda amesema Mitaala mipya ya Elimu ya Awali, Msingi,
Sekondari na Elimu ya Ualimu itaanza kutumika baada ya Sera ya Elimu na
Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kupitishwa na Mamlaka za Maamuzi.
Prof.
Mkenda amesema hayo leo Agosti 18 ,2023 jijini Dodoma wakati
akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo ameeleza kuwa tarehe rasmi ya
kuanza kutumika kwa mitaala hiyo itatangazwa mara baada ya kupitishwa
kwa Sera hiyo na kwamba itakapopitishwa utekelezaji utaanza kwa awamu
Kiongozi
huyo ameongeza kuwa rasimu iliyopo inapendekeza watoto waliopo darasa
la Tatu Mwaka huu 2023 ndio watakaosoma mpaka darasa la Sita, hivyo wale
waliopo katika madarasa ya Nne, Tano na Sita wataendelea kusoma mpaka
darasa la Baba.
"Hatima ya yote utekelezaji huu unategemea
mamlaka ya nchi itakaposema tuanze, matumaini yetu ni makubwa kwamba
rasimu hii itapita na siku ya kutangazwa kuanza kwa utekelezaji itakuwa
ni siku kubwa katika kuelekea mageuzi ya elimu nchini" amesisitiza Prof.
Mkenda
Aidha Prof. Mkenda ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa
Ufadhili wa Samia Skolashipu ambapo amesema Wanafunzi wanaonufaika
wasipofikisha GPA 3.8 wataondolewa katika ufadhili huo na kuwekwa kwenye
mikopo, lengo ni kuwataka wanafunzi hao kuendelea kusoma kwa bidii na
kufanya vizuri.
Amesema kuwa Wanafunzi hao wamesaini mkataba na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambao pamoja na
mambo mengine unawataka kuhakikisha wana endelea kupata matokeo mazuri
na kusomea masomo ya sayansi, Hisabati, Uandisi na Elimu tiba na
hawaruhusiwi kubadilisha fani zisizokuwa za Sayansi.
"Ule
mkataba unakupa masharti, umeanisha majukumu yako wewe si umefaulu
vizuri sana, basi tunatarajia ukienda Chuo Kikuu uendelee kufaulu
vizuri, ukishuka tutakuondoa kwenye ufadhili tulakupeleka kwenye
mikopo" Alibainisha Prof. Mkenda.
Kuhusu ufundishaji wa somo la
dini katika shule za Msingi na Sekondari Prof. Mkenda ameeleza kuwa
ukusanyaji wa maoni ya Sera mpya yalihusisha Viongozi wote wa dini
kutoka madhehebu mbalimbali ya dini ambao kwa kiwango kikubwa
wamechangia katika mapitio ya Sera pia wamehusishwa katika Uandaaji wa
mitaala.
"Katika kipindi hiki mageuzi ya Elimu yamekuwa
shirikishi, wazi na ya muda mrefu, mwezi Mei mwishoni tulikuwa na
Kongamano na lilirishwa mubashara, lilikuwa na Maaskofu, Mashehe,
Mapadri Wanazuoni wa dini ya Kiislam na Kikristo walishiriki kwa
pamoja". Alieleza Prof. Mkenda
Aidha amesema mitaala
inayohusiana na dini inaandikwa na wataalam wa dini wanaoletwa na
Taasisi za dini hizo, na kwamba yeyote anaehitaji kuisoma mitaala na
mihtasari hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 18,2023 jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu kuanza kutumika Mitaala mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu kuanza kutumika Mitaala mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu leo Agosti 18,2023 jijini Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...