Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kassanda amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata wahalifu na badala yake washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kwaajili ya kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wanaokamatwa.

DC Kassanda ametoa agizo hilo jana Jumatano Agosti 16, 2023 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Bujashi akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo Wilaya ya Magu pamoja na kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi.

Akizungumza na Wananchi wa Bujashi DC Kassanda amewaasa wakazi wa Kata hiyo kuacha tabia hiyo mara moja kwani ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi kwasasabu vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwaajili ya kutatua changamoto hiyo hivyo wananchi wanapokamata mhalifu wanatakiwa kutoa taarifa katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

Aidha amewahimiza wananchi wa Magu kulinda na kuthamini miradi ya maendeleo iliyopo Wilayani humo ili iendelee kunufaisha wananchi na kuunga mkono juhudi za serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katika hatua nyingine DC Kassanda amewataka wazazi kuendelea kusimamia suala la maadili ya watoto haswa kukemea tabia ya utoro shuleni kwa watoto .

Kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hao Dc Kassanda amewataka wananchi kuziwashilisha kwa viongozi wao kuanzia ngazi ya Kata ili uongozi wa Wilaya uzifanyie kazi.

DC Kassanda anaendelea na ziara ya kukagua shughuli za miradi ya maendeleo ambapo anatarajia kutembelea kata 25 za Wilaya ya Magu kuanzia tarehe 16-25/08/2023.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...