Na Mwandishi Wetu, Same
SHULE ya Msingi Same mkoani Kilimanjaro imepokea msaada vitu mbalimbali muhimu kwa ajili ya wanafunzi wasioona katika shule hiyo wenye jumla ya thamani ya Sh.milioni moja kutoka Mgahawa wa Ustaadhi Food Restaurant.
Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya Mgahawa huo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika program ya 'Tabasam na Mama'
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Mgahawa wa Ustadhi Food Restaurant Radhia Awadhi Daffa amesema ametoa msaada huo kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa anaguswa na matatizo ya watoto wenye uhitaji hapa nchini kwa kuwachangia gharama za matibabu na kuwapatia misaada mbalimbali.
"Ustaadhi Food Restaurant tumeamua kuendeleza program ya Tabasam na Mama kwa kuchangia mahitaji muhimu kwa wenye uhitaji na program hii kwetu itakuwa endelevu"amesema Radhia
Mbali na hayo pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same na Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwafikia watu wenye uhitaji.
Aidha Mkurugenzi huyo ametoa mwito kwa wakina mama kuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.
Awali Mkuu wa shule ya Msingi Same Elimu ya Awali Hurumar Mgonja amemshukuru Radhia Awadhi kwa msaada aliotoa kwa watoto hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...