Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurace Dkt.Elirehema Doriye (wa pili kutoka kushoto)akipokea Tuzo ya Superbrands Afrika Mashariki kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Superbrands Jawad Jaffer (wa tatu kutoka kushoto) katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa NIC Insurance Jijini Dar es Salaam (wa kwanza kushoto ) Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Karimu Meshack na mwisho kutoka kushoto ni kutoka kampuni ya Superbrand.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurace Dkt.Elirehema Doriye akipokea Tuzo ya Superbrands Afrika Mashariki kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Superbrands Jawad Jaffer katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa NIC Insurance Jijini Dar es Salaam.

*Dkt.Doriye aahidi neema zaidi ya kutoa bima kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu
NIC Insurace imepokea Tuzo kutoka kampuni ya Superbrands Afrika Mashriki ikiwa ni matokeo ya kazi wanazofanya katika kuhudumia wateja wake kwa ufanisi.

Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Dkt. Elirehema Doriye amesema wataendelea kuwa na ubunifu wa bidhaa ambazo zitagusa watu wote kupata bima mbalimbali na kuweka kuwa salama wakati wote wa shughuli zao.

Amesema cheti hicho cha Superbrands kinaonyesha kuwa utendaji kazi wa NIC Insurance kuwa bora kwa kutoa huduma pamoja na ubora wa bidhaa na namna mteja anavyoridhika na huduma zinazotolewa.

"Leo ni siku ya kipekee kwetu kama NIC Insurance kwani ni mara ya kwanza kupokea cheti/tuzo hii ya Superbrands hii inaonyesha namna tunavyofanya kazi vizuri katika kuwahudumia wateja mbalimbali kwetu huu ni mwanzo tu tutaendelea kutoa huduma Bora Kwa kila Mtanzania”amesema Dkt.Doriye

Ameongeza kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni inayomilikiwa na serikali kupata cheti hicho haya ni mafananikio kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Hii inaonyesha mafanikio na mikakati ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuvutia wawekezaji ni pamoja na kuwa kampuni imara ya bima ya kuwamudu wawekezaji ambapo hiyo ndio nafasi ya NIC Insurance" amesema Dkt.Doriye

Amesema kufuatia utafiti huru uliofanywa na kampuni ya Superbrands wa kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ndio umetoa mwanga wa namna bima hiyo inavyofanya kazi na kuwatofautisha na kampuni nyingine za bima nchini.

Aidha Doriye Ameongeza kuwa wanatarajia kuboresha mifumo zàidi matumizi ya teknolojia ili kuwafikia wananchi kila sehemu..

Kwa upande wake Meneja Miradi kutoka kampuni ya Superbrands Jawad Jaffer amesema upatikanaji wa tuzo hiyo kwa NIC Insurace walifuata vigezo ikiwemo kufanya utafiti kwa Nchi za Afrika Mashariki.

Amesema wameweza kuwafikia wananchi katika nchi hizo na kuwauliza kuhusu huduma za bima wanazotumia na kuona watu wengi wakivutiwa zàidi na huduma zinazotolewa na NIC Insurance.

“Ili kutoa hiki cheti cha Superbrands kwa taasisi na mashirika tunafanya utafiti wa kutosha ikiwemo utoaji wa huduma na ubora wa bidhaa kwa watumiaji katika sekta ya bima utafiti ulioonyesha watu wengi kuvutiwa na huduma zinazotolewa na NIC Insurance" amesema Jaffer

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...