Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza baada kushuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Everisto Longopa (kulia) ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ya vitendea kazi Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Balozi Prof. Kennedy Gaston. Hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Makao Mak uu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Septemba 20, 2023.Hafla hiyo pia ilihusisha kumuaga Dkt Longopa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Everisto Longopa (kulia) ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ya vitendea kazi Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Balozi Prof. Kennedy Gaston.
Aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Everisto Longopa (kulia) ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Balozi Prof. Kennedy Gaston.

Viongozi hao wakiwa katika picha za pamoja na baadhi ya viongozi wa menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo.


PICHA NA RICHARD MWAIKENDA


Na Mwandishi Maalum


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amemtaka Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikaki Mhe. Balozi Prof. Kennedy Gaston kuhakikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, inaendelea kupata hati safi ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalia ( CAG).


Amesisitiza kuwa jambo hilo la Ofisi kuendelea kuwa na hati safi linaweza likawa la kushangaza lakini ni jambo la msingi na muhimu sana kwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali jambo ambalo linakwenda sambamba na usafi na maadili ya Ofisi.


Ameyasema hayo siku ya jumatano ( septemba 20,2023) wakati wa hafla ya kumkaribisha rasmi na kukabidhiwa Ofisi Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Balozi Prof. Kennedy Gaston, hafla hiyo, iliyofanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, pia ilihusisha kumuaga aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu.


Dkt. Evaristo Longopa aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alimkabidhi Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Balozi Prof. Kennedy Gaston Ofisi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Pamoja na Nyaraka mbalimbali muhimu zinazosimamia utekelezaji wa Majukumu yake.


Mhe. Feleshi amebainisha kuwa katika kipindi chote cha takribani miaka mitano ambayo Dkt. Longopa aliyotumikia kama Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali yapo mambo mengi ambayo ameyatekeleza na kuyasimamia kwa karibu sana.


“Tunamshukuru sana Dkt.Longopa, kati ya vitu hata nikisahau, yeye na timu yake ya manejiment, anaondoka tukiwa na hati safi kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, unaweza ukashangaa , lakini hili ni eneo muhimu sana kulilinda ( hati safi) pamoja na maadili na usafi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) akasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Feleshi.


Aidha Pamoja na kumtaka Naibu Mwanasheria Mkuu Gaston kuhakikisha Ofisi inaendelea kupata hati safi, pia amemtaka pamoja na mambo mengine ya kiutendaji yanayomhusu kama Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kuhakikisha kwamba Nakala za Mikataba ambazo zimekwisha sainiwa na wizara na Taasisi baada ya kufanyiwa upekuzi zinarudishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


“Nakuona unakazi nyingi kuliko mimi, kwa sababu watu au wadau wetu watakaoshindwa kunipata mimi kwa sababu yoyote ile watakuja kwao si semi kwamba utafanya kazi kwa saa 24 lakini hili linaweza kutokea kwa mazingira ya Ofisi yetu” akabinisha
Akasisitiza kuwa ni muhimu Ofisi kuwa na nakala ya mkataba au mikataba iliyosainiwa ili kuiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatilia.


Katika hatua nyingine, Jaji Feleshi amemtaka pia Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof Gaston kuendeleza juhudi za kuboresha hali bora za watumishi, matumizi ya mifumo ya tehama huku akiwataka watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumpatia ushirikiano Naibu Mwanasheria Mkuu Pamoja na kudumisha upendo, mshikamano na umoja na kuombeana.


Kwa upande wake Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Balozi Prof. Kennedy Gaston ameshukuru kwa mapokezi mazuri na ukarimu alioonyeshwa na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwamba anashukuru kuwa sehemu ya familia ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


Amewashukuru watumishi wote kwa kuahidi kumpatia ushirikiano, huku akiwataka kutokuwa na hofu wala uoga na kwamba jambo la msingi ni kazi iendelee.


Akizungumza kwa niaba ya watumishi wote, Bi. Esther Cheyo Katibu Sheria Mkuu, alimuhakikishia ushirikiano wa watumishi wote katika utekelezaji wa majukumu yake.


Kwa upande wake Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole akizungumza kwa niaba ya Menejiment amesema Menejimenti itampatia ushirikiano na kuahidi kufanya naye kazi kwa karibu kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.


Naye Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Dkt. Evaristo Longopa pamoja na kutoa shukrani zake kwa ushirikiano ambao watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu walimpatia katika kupindi chote alichofanya kazi nao, amewahimiza watumishi hao kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na kujituma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...