MKUU wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi leo Septemba 23, 2023, aliungana na wananchi wa kata ya Kiburugwa katika tarafa ya Mbagala wilayani Temeke, kufanya usafi katika zahanati ya Kingugi.

Ufanyaji usafi umeratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika kata ya Kiburugwa chini ya Sheikh  Saidi Kiduka kiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Maulid ya Mtume Muhammad (SAW).

Akizungumza mara baada ya usafi huo na kuwashukuru uongozi wa BAKWATA, zahanati, kata, mtaa na wananchi kwa ujumla Mkuu wa Wilaya Matinyi amesema, "Ndugu wananchi tuendelee kufanya usafi kwa ajili ya mazingira yetu na afya zetu na zoezi hili liwe endelevu."

Kwa upande wake Sheikh  Kiduka amesema usafi ni jambo muhimu katika jamii ambalo hata Mtume Muhammad (SAW) pia alilisisitizia na kumnukuu katika maneno yake akisema "Uislamu ni usafi".

Wakati huo huo Diwani wa kata hiyo, Fatma Shija, naye ameshiriki kufanya usafi akiambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa ngazi ya kata na mtaa na hali kadhalika wenyeviti na watendaji wa kata na mitaa.

Baada ya kufanyika kwa usafi huo Diwani Shija alimchukua Matinyi katika ziara fupi kumwonesha changamoto za miundombinu ya barabara, mifereji na mitaro katika kata hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya amesema amejionea mwenyewe na amezipokea changamoto hizo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...