Na.Khadija Seif Michuziblog

SIKU CHACHE Mara baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Kutangaza kuufungia kuchezwa katika vituo vyote vya redio na televisheni wimbo wa ''Amkeni" wa Msanii wa Hip-hop Emmanuel elibariki maarufu "Ney wa Mitego" hatimae wamfikisha kituo cha polisi (Central) Jijini Dar es Salaam .

Akizungumza machache na Wanahabari Leo Septemba 06,2023 Ney wa Mitego kabla ya kuingia kikaoni akiwa ameambatana na Mwanasheria wake Jebra Kambona amesema ameitika wito mara baada ya kupokea ujumbe kuwa anatakiwa kufika kituoni hapo kwa Mahojiano baada ya kufunguliwa shtaka la wimbo wake huo uliokiuka maadili ya Kitanzania.

"Ukiwa sauti ya Watu kuja sehemu kama hii ni kawaida mimi ni sauti ya watu acha nikawasikilize nitakuwa na cha kuongea lakini kwa sasa sina, nimeambiwa tu ni wimbo wangu wa 'Amkeni ' kwahiyo nataka nikajue umefanya nini, kuna tatizo gani.''

Hata hivyo Ney wa Mitego alikosa cha kujibu maara baada ya kuulizwa swali na Wanahabari kuwa anatunga nyimbo zenye utata na kuvuka maadili na kukashifu viongozi kwa kile kinachoelezwa kuwa huku anategemea zaidi huruma ya watanzania ambao wengi ni Mashabiki zake katika kumtetea kwenye Masakata mbalimbali yanayomfika kupitia tasnia yake ya Muziki wa Hip-hop.


Pia Mapema mwezi Septemba Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Lilizuia vibali cha Msanii huyo kutofanya Show Mkoani Njombe ambapo alitarajiwa kufanya show Septemba 02,03,2023 .


Nae Mwanasheria wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Christopher Kamugisha ametolea ufafanuzi wa kesi ya Msanii huyo kuhusishwa na baraza hilo kufikishwa kwake kituoni Leo kuwa mara kadhaa amekuwa akipewa wito wa kufika Basata lakini  hajaitika wito mara 02 pindi alipoitwa na Walezi hao.


"Naomba nitoe ufafanuzi kuwa Basata haihusiki na swala la msanii huyo kufikishwa kituoni hapo (central polisi ) na tulituma muito mwingine kupitia Mwanasheria wake Siku ya ijumaa saa 4 hatujajua kama atafika tusubiri."



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...