MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula,unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023, na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo anayeshuhulikia Masuala ya Kimataifa  wa Norway Mhe.Anne Beathe Tvinnereim na (kushoto kwake) Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt.Agnes Kalibata.(Picha na Ikulu)


MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutoa Mada juu ya nafasi ya Mwanamke katika Kilimo, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023(AGRF) linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023.(Picha na Ikulu)

WASHIRIKI wa Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa jengo la Mikutano la Kimataifa la Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, kabla ya kuaza kwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) uliyofanyika leo 6-9-2023 katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe. Ummy Nderiananga na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) lililofanyika leo 6-9-2023, katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...