Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko imefanya ziara ya Ukaguzi wa kikosi cha Mbwa katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikosi hicho katika eneo hilo, kuhakiki ufanisi wake na kuboresha utendaji


Akizungumza na Maafisa wa Uhifadhi na Askari wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam na Pwani pamoja na kikosi cha K9 kinachojumuisha Askari Wenye mafunzo maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa nyara za maliasili katika viwanja vya ndege na bandari Septemba 15, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mej. Jen. (Mstaafu) Semfuko amewasisitiza wahifadhi hao kuongeza Ubunifu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwa na mahusiano mazuri katika shughuli zao Ili kuzilinda rasilimali za nchi.

"Ninyi ndio waanzilishi na ndio mtakuwa viongozi wakuu hapo baadae wa Unit hii hivyo TAWA tunatakiwa kuwa wabunifu wa viwango vya juu” amesema

Nae Naibu kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mlage Kabange amesema wameridhishwa na kazi nzuri ya udhibiti na ukaguzi wa nyara zinazotoka na kuingia hapa nchini, kwahiyo katika eneo la uwanja wa ndege jukumu hili linafanyika vizuri kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za ulinzi na Usalama katika kudhibiti wa utoroshaji wa nyara nje ya nchi.

"Mabadiliko haya chanya hayajaja kwa bahati mbaya, kunasababu ambazo zimefanya tuwe na mabadiliko makubwa na chanya kama haya ni Uadilifu, Uwajibikaji, Nidhamu ya hali ya juu, Mikakati na timu work" tunategemea juhudi zaidi na weledi zaidi katika kutekeleza majukumu yenu, alisema mmoja wa wajumbe wa bodi Prof. Jafari Kideghesho.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja Cha Ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere, Lugano Mwansasu ameeleza mafanikio yanayopatikana katika udhibiti wa nyara za serikali viwanjani hapo kupitia TAWA.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...