Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Dar es salaam.

Askari wa Jeshi la Polisi waliotimiza miaka tisa (09) kazini depo yam waka 2013/2014 (H3) waguswa na kampeni ya namthamini inayoendeshwa na kituo cha Televisheni na Redio cha East Afrika ambacho kinalenga kuwasaidia Watoto wa kike walioko mashuleni hapa nchini kupata taulo za kike.

Akiongea mara baada ya kukabidhi taulo hizo mkufunzi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Daer es salaam (DPA) ambae aliambatana na askari hao Mkaguzi wa Jeshi la Polisi INSP Lule Mlay amebainisha kuwa askari hao wameungana ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa kufikia miaka tisa ya utumishi ndani ya Jeshi hilo huku akisema wametoa taulo za kike ili kusaidia kundi la mabinti walioko mashuleni.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Digna Miho amesema wameamua kumshukuru Mungu kwa kulikumbuka kundi la mabinti waliopo mashuleni huku akibainisha kuwa anafahamu changamoto za mabinti wanapokuwa katika mizunguko ya mwezi (hedhi).

Nae Mwanafunzi wa kozi ya Mkaguzi msaidizi wa Polisi Abel Paul amesema mabinti wanahitaji kusoma bila kukutana na vikwazo kwa kutambua hilo waliona waungane na kampeni ya namthamini kuwasaidia mabinti kwa kutoa taulo za kike.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...