Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Fedha Utawala na Mipango wa chuo hicho, Dkt. Lucas Mwisila akizungumza ameyasema hayo Septemba 8, 2023 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Jukwaa hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo hich Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Dawati la Jinsia vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka wizara ya maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na makundi maalum, Gift sowoya akizungumza katika hafla hiyo

Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni OCS Sarah Bundara akizungumzia uwepo wa madawati ya Jinsia chini kulivyoleta matokeo chaya kupambana na ukatili wa kijinsia.

Picha ya pamoja (PICHA NA: HUGHES DUGILO) Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Chuo cha Bahari Dar es Salaam, (DMI), kimezindua Dawati la Kijinsia Chuoni hapo litalojihusisha kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi na watumishi katika chuo hicho.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa Dawati hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Fedha Utawala na Mipango wa chuo hicho, Dkt. Lucas Mwisila amesema uwepo wa Dawati hilo ni hatua kubwa iliyofikiwa na DMI katika kuhakikisha changamoto za ukatili wa Kijinsia chuoni hapo zinashughulikiwa.

Ameeleza kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakiathiri vijana wengi kwenye jamii, na kwamba kwa mwanafunzi inasababisha athari katika shughuli zake za kitaaluma.

Dkt. Mwisila ameyasema hayo Septemba 8, 2023 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Jukwaa hilo iliyofanyika katika Chuo cha DMI Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, mratibu wa Dawati la Jinsia vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka wizara ya maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na makurdi maalum, Gift sowoya, amesema kuwa kuanzishwa kwa Dawati hilo chuoni hapo kunaongeza idadi ya Madawati hayo kufikia 421 yaliyopo katika Taasisi mbalimbali za Elimu hapa nchini.

“Niwapongeze Chuo cha DMI kwani wamekuwa miongozi mwa Taasisi zilizotekeleza mwongozo huu kwani mpaka sasa tuna Madawati 420, na hili tuliloanzisha leo hapa DMI tumfikia Madawati 421.

“Dawati hili halipo tu kwa wanafunzi peke yao, bali litashughulika na watu wote wanaofanyakazi katika chuo hiki wakiwepo walimu. Naomba wote mlitumie bila kubagua” amesema Sowoya.

Naye, Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni OCS Sarah Bundara amsema uwepo wa Madawati ya Jinsia kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na ukatili wa kijinsia ukizingatia tatizo hilo limekuwa kubwa kwenye jamii kutokana na uwepo wa watoto wa kiume kuhusishwa na vitendo hivyo.

“Tumekuwa tukipokea kesi nyingi za ukatili kwa watoto na watu wazima pia, kesi hizi zipo, na sasa hata watoto wa kiume wameingia kwenye changamoto hiyo.

“Watoto wa kiume nao wanahitaji kulindwa kama ilivyo kwa watoto wa kike, kwa sababu mazingira na mabadiliko ya teknolojia imepelekea kuingia katika ukatili bila wao mwenyewe kujua” amesema OCS Bundara.

Ameeleza kuwa katika madawati yao wamekuwa wakipokea kesi za uwepo wa rushwa ya ngono vyuoni kutokana na sababu mbalimbali, ambapo amekipongeza Chuo cha DMI kuanzisha Dawati hilo litalowafikia wanafunzi kueleza vitendo vya ukatili wa kijinsi wanavyokabiliana navyo ikiwemo vitendo vya rushwa ya ngono.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...