Na John Walter-Manyara
Mkuu
wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameanzisha mpango wa kusikiliza kero
za wananchi kwa kuwafuata kwenye Mitaa na vijiji vyao kupitia ofisi
inayotembea (Mobile office) ili waweze kuwafikia kwa wingi zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo septemba 6,2023 amesema kuanzia kesho
alhamisi septemba 7,2023 ataambatana na idara, taasisi zote za serikali
zilizopo katika wilaya ya Babati kusikiliza na kuzitatua kero zote
zilizopo.
Pia, DC Twange amewataka watumishiwote wa serikali kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita katika kuwahudumia wananchi.
Amewataka
Madiwani, Wenyeviti wa mitaa, vijiji na watendaji wa serikali katika
kata vijiji na mitaa kuwahimiza wananchi kufika katika maeneo mkutano
utakapofanyika.
Twange amewasihi wananchi kutoa kero, changamoto na matatizo yao bila hofu yoyote kwa kuwa serikali ipo kwa ajili yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...