NA MASHAKA MHANDO, Lushoto

MKUU wa wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro ameagizwa kuhakikisha anachukua hatua za haraka kurejesha amani katika kata ya Lunguza kufuatia vurugu za wakulima na Wafugaji.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba mwishoni mwa wiki, kufuatia wananchi kulalamika kwamba Wafugaji katika eneo hilo  wanalishia mifugo yao mazao ya wakulima.

Kindamba alisema serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, haiwezi kuona wananchi wanataka kulima mazao yao lakini kuna watu wengine wanawakosesha amani, haitawwzekana.

"Wakati wangu nikiwa Mkuu wa mkoa, hakuna ambaye haki yake itapuuzwa, wale wenye kuwaumiza wenzao kwa kuchukua Sheria mkononi naviagiza vyombo vya dola kusimamia Sheria asionewe mkulima kwasababu hana fedha," alisema na kuongeza,

"Limetajwa hapa boma la Mlandizi na Iheku DC katazame na chukua hatua lisije likakuharibikia, ukisikia wananchi wanalalamika namna hii, yapo maneno ya kiswahili yanasema panapofuka moshi upo moto chini unawaka,".

Mkuu wa mkoa aliwataka viongozi wa wilaya ya Lushoto kila mtu kwa nafasi yake wahakikishe wanajitasmini na kuchukua hatua mahususi na madhubuti za kuondoa manung'uniko na malalamiko ya wananchi ili amani katika eneo hilo iweze kurejea.

"Rais (Dkt Samia Suluhu Hassan) katuleta huku akituamini kuwa tutakuwa mstari wa mbele katika utatuzi wa kero za wananchi hilo ndilo lengo la serikali," alisema.

Mbunge wa Jimbo la Mlalo Rashid alisema mgogoro uliopo katika kata hiyo baina ya wakulima na Wafugaji umefanya miradi mikubwa ambayo Rais Dkt Samia ameleta fedha, wananchi hawaoni hayo kutokana na mgogoro huo.

"Tunaomba serikali mmalize mgogoro huu, Kijiji Cha Lunguza na Kivingo vyote vimo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi, Rais Dkt Samia katoa Bilioni 1.1 kwa ajili ya skimu lakini ufugaji ni tatizo wananchi hawaoni uwekezaji huu kutokana na tatizo hilo," alisema.

Awali kabla ya Mkuu wa mkoa kuzungumza wananchi wa kata hiyo walimweleza kwamba Lunguza kuna mgogoro mkubwa baina ya wakulima na Wafugaji kiasi cha watu kupigwa na damu kumwagika.

Abdul Omar mkazi wa Kijiji Cha Lunguza alimweleza mkuu wa mkoa kwamba wafugaji ndiyo tatizo katika eneo hilo na wanapokwenda kwa viongozi wanashindwa kupata haki zao na wafugaji kutamba kwamba wananguvu kuliko mkulima.

"Wafugaji wanapolisha ng'ombe zao mazao yetu tunapokwenda kwa vyombo vya dola tunaambiwa tukakamate mifugo, wakati mfugaji anapolisha shamba huyo huyo anakukata na sime lake," alisema.

Amina Omari akizungumza kwa masikitiko alisema kwamba wanapotoa malalamiko kwa viongozi hayatatuliwi hatua ambayo kwasasa wanashindwa kulima wakiogopa Wamasai ambao wanaingiza mifugo yao katika mashamba.

Alisema Kijiji chao kimewekwa katika matumizi bora ya ardhi lakini wafugaji wamekua wakiuka Sheria kwa kuingiza mifugo yao mashambani na wanapokwenda mahakamani wanashinda kesi kutokana na kuwa na fedha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...