Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi-Auckland New Zealand

Askari wa Kike kutoka Nchini Tanzania wameshiriki Mkutano wa mwaka 2023 wa Mtandao wa Polisi Wanawake Duniani (IAWP) Nchini New Zealand.

Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo" Refresh, Renew,Refocus umefunguliwa September 17,2023 mji wa Auckland.

Aidha Mkutano huo umeudhuriwa na mataifa kama vile Tanzania,Ghana na Africa Kusini.

Itakumbukwa mwishoni mwa mwezi Julai  Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano kama huo kwa ukanda ya Afrika uliyofanyika jijini Dar es salaam na kuleta matokeo makubwa ya kiutendaji kwa maafisa na askari wa kike ambao walishiriki na mada mbalimbali kufundishwa lengo likiwa kuwaongezea uwezo na maarifa ya kiutendaji.

Mkutano huo uliofunguliwa leo septemba 17,2023 katika mji Auckland Nchini New zealand unaoambatana na mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wa kike, sambamba na kutoa fursa na kutengeneza mtandao wa mawasiliano kwa wasimamizi wa sheria.

Mbali na hilo Ujumbe huo kutoka Tanzania uliongozwa na Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda wa kamisheni ya Utawala na rasilimali watu umetumia mkutano huo kutangaza utalii na vivutio vya kitamaduni vilivyopo Tanzania.

Mkutano huo hutahitimishwa Septemba 21,Mwaka huu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...