Na Shalua Mpanda -TMC

MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Mobhare Matinyi amefanya ziara ya kukagua uchafuzi wa Mazingira katika mfereji mkubwa unaounganisha kata tatu ndani ya Wilaya hiyo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo,Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke ameonesha kuchukizwa na hali ya uchafuzi wa mazingira ikiwemo utupaji wa takataka ndani ya mfereji huo mkubwa ulioigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 18 kuutengeneza.

Amesema wananchi wanatakiwa kuuchukia uchafu na kujali hali zao pamoja na kuthamini fedha za Serikali zinazotolewa kutengeneza miundombinu mbalimbali.

"Mfereji huu tuliufanyia ukaguzi mwezi uliopita tukakuta kuna changamoto ya kujaa uchafu,tukaielekeza Manispaa na wakatafuta mkandarasi wa kufanya kazi hii....makandarasi amelipwa zaidi ya milioni 15 kufanya kazi hii lakini akisafisha akisogea mbele huku nyuma watu wanatupa taka, "alisema Matinyi

Nyambiga Masila mkazi wa Keko Magurumbasi 'B" ametoa rai kwa viongozi wa Serikali za mitaa kuungana pamoja kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira.

"Mfereji huu katika kata hii tu ya Keko umepita kwenye mitaa mitano ambayo viongozi wake wakiungana kwa pamoja na kuhamasisha Wananchi kutunza mfereji huu,changamoto hii itaisha".Alisema Mkazi huyo.

Ziara hii inafanyika katika kipindi hiki ambacho Dunia inaenda kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani Septemba 16 ambapo manispaa ya Temeke ilizindua wiki ya usafi Septemba 11 na maadhimisho hayo ya Siku ya Usafi duniani kiwilaya yatafanyika viwanja vya Zakhem Mbagala ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...