Na.Damian Kunambi, Njombe

Kufuatia adha waliyokuwa wakiipata Wananchi wa kitingoji cha Chimbo kilichopo katika kijiji cha Amani kata ya Mundindi wilayani Ludewa mkoani Njombe ya kutembea umbali wa zaidi ya Km. 13 kufuata huduma ya afya, hatimaye wananchi hao wanaenda kuondokana na adha hiyo baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa zahanati katika kitongoji hicho kwa kutoa fedha kiasi cha sh. Mil. 50.

Wananchi hao wameonyesha shangwe nyingi wakati mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva akizindua zahanati hiyo na kusema kuwa zahanati hiyo itakuwa ukombozi kwao kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakifia njiani kutokana na kuchelewa kufika hospitali kupatiwa huduma hiyo wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha hizo sambamba na mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga kwa kutoa mifuko ya saruji kupitia mfuko wa jimbo pamoja na mfuko wake binafsi.

Alatukolela Kihombo ni miongoni mwa wananchi hao amesema awali wakati wakihamasishwa kufanya maendeleo hayo ya ujenzi na mwenyekiti wa kitongoji hicho Ally Mshega walikuwa hawamuelewi lakini sasa baada ya serikali kuunga mkono jitihada zao hizo na kukamilisha zahati hiyo wameona na kuelewa nia ya mwenyekiti wao kwani kitongoji hicho kina mwingiliano wa watu wa maeneo mbalimbali kutokana na uwepo wa shughuli za uchimbaji madini zinazoendelea kitongojini hapo pamoja na kilimo.

Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya aliwapongeza wananchi kwa jitihada za kuchangia maendeleo walizozifanya kwa kuchangia fedha kiasi cha zaidi ya sh. Mil. 8 huku thamani ya nguvu kazi ikiwa ni zaidi ya sh. Mil. 9 kitu ambacho kimepelekea serikali kuunga mkono kwa kutoa kiasi hicho cha Sh. Mil. 50 ambazo zimewezesha kukamilisha ujenzi huo.

"Serikali ya Rais Dkt. Samaia Suluhu Hassan ipo bega kwa bega na nyie katika kuleta maendeleo hapa wilayani kwetu Ludewa, licha ya fedha hizi zilizotumika katika zahanati hii lakini pia kuna fedha nyingi sana zimeletwa za miradi ya elimu, barabara, afya na miradi mingineyo hivyo tuendelee kuwaunga mkono viongozi wetu ili tupate maendeleo zaidi", amsema mkuu wa Wilaya Mwanziva.

Gervas Ndaki ni katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa amesema kitendo cha maendeleo kilichofanywa na wananchi hao ni kitendo cha kuigwa kwani imezoeleka kuwa ujenzi wa zahanati hufanyika kwa ngazi ya kijiji pekee lakini wanakitongoji cha Chimbo wameonyesha kuwa maendeleo yanaweza kufanyika hata katika ngazi ya kitongoji.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Sunday Deogratius amesema kitongoji hicho kitakuwa ni kitongoji cha mfano kwa vitongoji vingine ikiwemo katika vikao vya baraza la madiwani ili mfano huo uweze kuigwa katika maeneo mengine pia.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...