Na Damian Kunambi, Njombe

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa Gervas Ndaki amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuona namna ya kuwajengea shule shikizi wanafunzi wanaotoka  katika kitongoji cha Chimbo kilichopo katika kata ya Mundindi wilayani Ludewa mkoani Njombe ili kuwapunguzia umbali wa zaidi ya Km. 13 wanaotembea wanafunzi hao kwenda kufuata elimu kwenye makao makuu ya Kijiji cha amani, huku wengine wakiombewa na wazazi wao kuishi katika familia za watu baki.

Katibu ndaki ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zahanati ya kitongoji cha Chimbo kilichopo katika kijiji cha Amani kata ya Mundindi baada ya wananchi kuanzisha ujenzi wa zahanati hiyo na kukamilishwa na serikali kwa lengo la kuepuka umbali huo kufuata huduma ya afya na kusema kuwa wanafunzi nao wanapaswa kufikiriwa katika hilo.

" Niwapongeze kwa kujenga zahanati hii lakini pia kuna umuhimu wa kujenga shule pia ili tuwaokoe na hawa watoto wetu wanaotembea umbali mrefu kwenda shuleni, maana nimesikia kuna baadhi ya wazazi mmewekeza watoto wenu kwa watu huko jirani na shule ili kuepusha wasitembee umbali mrefu, sasa niwaombe kwa nguvu hii iliyotumika kujenga zahanati itumike pia katika kujenga shule shikizi".

Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratius amesema amelipokea hilo na kwenda kulifanyia kazi huku Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri Wise Mgina akisema tayari mchakato wake umekwisha anza ambapo Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ametoa ahadi ya kuchangia bati zitakazotosha madarasa mawili.

Hata hivyo kwa upande wa wananchi wamedai kuwa tatizo hilo la umbali limekuwa ni kikwazo kwa wanafunzi cha kutofika mashuleni ambapo huishia mitaani na kupelekea watoto hao kuzagaa hovyo huku wengine wakiacha masomo.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...