Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dae es salaam.

Mkuu wa Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amefurahishwa na mwitikio mkubwa wa timu shiriki na wananchi wanaendelea jitokeza kufuatilia mashindano ya Polisi Jamii DPA Cup yanayoendelea katika viwanja vya chuo cha maafisa wa Polisi Vilivyopo kurasini jijini Dar es salaam.

Dkt Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati wa mchezo kati ya TM Rocket na Temeke youth uliomalizika kwa timu ya TM Rocket kushinda vikapu sitini na tano (65) kwa Hamsini na tanu (55) dhidi ya Temeke youth katika mchezo uliyochezwa mapema leo septemba 18 ,2023 katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) huku akitumia fulsa hiyo kuwakaribisha wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kufika na kutumia viwanja hivyo vipya na vya kisasa vilivyopo chuoni hapo.

Kwa upande wake mchezaji wa timu ya TM Rocket Emmanuel Samiri amesema ushindi wao umechagizwa na mazoezi na mbinu walizofundishwa na mwalimu wao kitendo kilichopelekea kuwachalaza wapinzani wao vikapu (67) kwa Hamsini na tano.

Nae mchezaji wa Temeke youth Paschal Benedicto amesema mchezo wao ulikuwa mgumu kutokana na wapizani wao ambao walikuwa bora Zaidi katika mchezo huku akiwaahidi mashabiki wake kuwa watafanya vizuri Zaidi katika michezo mingine inayofuata. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...