WAKAZI wa Kibaha wameshiriki katika mkutano wa kutoa elimu ya haki jinai kazi inayofanywa na Tume hiyo ambapo pamoja na mambo mengi wametoa maoni yao ikiwemo la Polisi Jamii waliopo kwenye kata kuondolewa kutokana na kazi wanayoifanya.

Vilevile wameomba kazi ya kunyonga wanaohusika na mauaji iundiwe kitengo chake badala ya kuacha jukumu hilo kwa Rais ili hali lipo ongezeko la watu wanaofanya vitendo hivyo kwa jamii.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Mailimoja mwishoni mwa wiki mmoja wa wananchi walioshiriki mkutano huo Hawa John alisema polisi hamii hao kutoka kwenye kata wamekuwa wakikaa polisi na kutumwa kukamata watuhumiwa.

" Hawa polisi Jamii wako sana kwenye kata unapofika kuelezea tukio lako polisi unaambiwa uwape hela ili wakamkamate mtuhumiwa hili jambo kwetu ni kero tunaomba Tume ilifanyie kazi" alisistiza.

Hawa pia alisema lipo suala la baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi kutowalinda watu wanaotoa taarifa za wahalifu linapaswa kuangaliwa Ili kulinda usalama wao kwani wapo wanaopelekewa taarifa kuhusiana na wahalifu lakini haohao Askari wanawataja watoa taarifa.

Naye Ramadhani Maulidi alieleza katika mkutano huo kwamba anatamani siku moja angeajiriwa na Serikali Ili akafanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji.

Alisema zipo taarifa zinazoelezwa kwenye vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi huku matukio ya mauaji yakiendelea ni wakati sasa Serikali kuliangalia suala hilo sambamba na kuajri watu wenye roho ngumu ambao watatekeleza adhabu ya kunyonga.

"Uanakuta mtu ameuwakwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani muda mrefu bila kunyongwa hilo haliwezekani kama mtu amekutwa na hatia ya kuuwa naye anyongwe, siyo unasikia wanaanza kusema haki za binadamu kwani yeye alipoku

Mjumbe waTume hiyo Dk Laurean Ndumbaro alisema kutosainiwa kwa adhabu ya kifo kwa watu wanaohukumiwa kutumikia adhabu hiyo kwa muda mrefu sasa kumesababisha uwepo wa mlundikano wa wafungwa na kwamba mapendekezo yao ni kuona suala hilo linangaliwa upya.

Prof. Edward Hosea ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai alisema.kuwa katika ufuatiliajj wao walibaini kwamba zipo sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho Ili kulinda haki za wananchi ikiwemo utitiri wa majeshi uliopo ambaounapaswa kuangaliwa na kuundiwa sheria upya.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...