Na Janeth Raphael - Michuzitv Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Charles Msonde amewataka Waratibu wa Mpango wa shule salama, Wasimamizi wa Usalama wa jamii wa Mikoa na Halmashauri, Walimu, Wazazi,Walezi na Jamii Kwa ujumla kushirikiana kikamilifu katika Malezi na Ulinzi wa Usalama wa Watoto.

Dkt.Msonde ameyasema hayo Leo Jijini Dodoma,wakati akifungua kikao Kazi cha Mafunzo ya kuwajengea uwezo Waratibu wa Mpango wa Shule salama na wasimamizi wa usalama wa jamii wa Mikoa na Halmashauri

"Malezi na ulinzi wa Mtoto ni jukumu letu sote hivyo Wazazi,walezi na jamii ishirikiane vyema na Shule wasiwaachie tu walimu kwani mtoto anaweza kupata changamoto Nyumbani,kwenye jamii ama shuleni hivyo ni muhimu kuwalinda Kwa pamoja".

Sambamba na hayo Dkt.Msonde amesema walimu wamepewa majuku ya kuhakikisha watoto wanakuwa na tabia njema,ujuzi na kuwa Mlezi Kwa Mtoto kwani mwalimu anaviona visa vingi vinavyowakumba watoto Kwa haraka zaidi kuliko hata wazazi wao.

"Mwalimu anakuwa wa kwanza kabisa kumuona mtoto anapokuwa na changamoto kwa sababu watoto wengi wanakuwa wawazi na huru kuwaelezea walimu wao changamoto wanazozipitia,

Na kuongeza kuwa "malezi ya watoto wetu yanatuhitaji sisi sote na jamii itambue umuhimu wa kuhakikisha wanashiriki kwa pamoja katika ulinzi na Usalama wa mtoto".

Amesema ili kutekeleza Mpango wa usalama wa mtoto ni lazima Kila Shule iwe na Baraza la watoto ili wawe na Fursa ya kujadiliana changamoto wanazokumbana nazo na wapewe uhuru wa kufikisha Kwa Mtu wanaomuamini.

Pia ametoa wito Kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kukumbuka kuwa wana wajibu wa kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa kulinda usalama wa Watoto.

Dkt.Msonde ameongeza kuwa wataalamu wengi hawawezi wakapatikana katika taifa lolote lile bila kuhakikisha kuwa sekta ya Elimu inaboreshwa na ndio maana Serikali imekuja na miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa kuboresha Elimu ya Msingi na Sekondari na ule Mradi wa kuboresha Elimu ya awali na Msingi (BOOST) ambao Serikali katika Mradi huo imewekeza Trilioni 1.5 Kwa miaka mitano.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa katika Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) Serikali imewekeza kiasi Cha Shilingi Trilioni 1.2 na Mradi huo umekuwa ukisaidia katika Ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Shule za sekondary ambapo kwa sasa wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha kwanza imeongezeka na Mradi wa SEQUIP umelenga kujenga Shule 1026 na katika Shule hizo 26 ni Shule maalum Kwa ajili ya Wasichana na Shule Moja itajengwa katika Kila Mkoa

Dkt.Msonde ametumua Fursa hiyo kuwaelekeza Wakurugenzi katika Halmashauri zote Nchini kuhakikisha midadi yote inatekeleza kama Muongozo uliyotolewa na Serikali inavyoelekeza na akisisitiza kuzingatiwa Kwa muda waliokubaliana katika kukamilisha Ujenzi wa Miradi hiyo.

Amesema katika kutekeleza Ujenzi wa Miradi hiyo ni muhimu kuwakumbuka watoto Wenye mahitaji Maalum na wasichani pia wakumbukwe ili kuwawezesha nao kupata elimu bila vikwazo vyovyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Elimu kutoka OR-TAMISEMI Vincent Kayombo amesema kuwa Maafisa wote wanaoshiriki Mafunzo hayo ni 630 hivyo Imani kubwa ni kuona matokeo ya Mafunzo hayo yanakwenda kuleta Tija katika Shule na jamii Kwa ujumla Kila mmoja akatambue umuhimu wa Malezi na ulinzi wa usalama wa Watoto.

Pia Kayombo amesema kuwa ongezeko la Vitendo vya Ukatili Kwa wananafunzi imesababisha Shule kuwa sio sehemu salama Kwa wakati Fulani ila kwa kutekelezwa Kwa mradi wa (SEQUIP) na Mafunzo kama haya ya Usalama yamesaidia Kwa kiwango kikubwa kurudisha Imani ya wanafunzi,Wazazi na walezi






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...