Na. Peter Haule, WF, Dodoma

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amewasilisha muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.

Akiwasilisha muswada huo bungeni jijini Dodoma Dkt. Nchemba, alisema kuwa muswada huo utaimarisha mazingira ya ununuzi na ugavi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara na kupunguza muda katika hatua na michakato ya zabuni.  

“Sehemu ya muswada huu unaainisha kuendelea kuwepo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, malengo na majukumu yake pia imeainisha nguvu ya kisheria Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kufanya uchunguzi, kupata taarifa, kutoa mapendekezo kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali au Afisa Masuuli wa Taasisi ya umma inayohusika na uchunguzi”, alieleza Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba alisema  kuwa Mamlaka hiyo itawasilisha matokeo ya uchunguzi kwa mtu au watu wenye mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu au hatua nyingine stahiki dhidi ya afisa au mtumishi na kuwasilisha taarifa maalumu kwa Waziri

Aidha imeainisha majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma ikiwemo kuomba taarifa, nyaraka na kumbukumbu ya aina yoyote, kuhusu mchakato wa ununuzi na ugavi, kutoa wito, kufanya uchunguzi na kuanzisha ukaguzi kwenye shughuli zinazohusiana na ununuzi na ugavi.

 

Pia muswada huo umeainisha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kupendekeza kwenye chombo chenye mamlaka kuhusu kusitisha utoaji wa fedha au kuzitaka taasisi kurejesha fedha zilizopotea, kubadilishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa Afisa Masuuli, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, Mjumbe wa kamati ya tathmini au afisa mwingine yoyote anayehusika katika mchakato wa ununuzi na uhamisho wa muda wa majukumu ya ununuzi ya taasisi kwenda taasisi nyingine au Wakala.

 

Vilevile vyanzo vya mapato ya Mamlaka ambavyo vitajumuisha fedha zitakazotengwa na Bunge, mikopo au misaada, mapato yatokanayo na bidhaa au huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma na fedha nyingine zozote zitakazopokelewa na Mamlaka kwa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akiteta jambo na  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo, baada ya kuwasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo (kushoto) akiteta jambo na Kamishna wa Sera za Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga (katikati) na Kamishna Msaidizi  Bw. Alex Haraba, baada ya kuwasilishwa bungeni muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023.


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...