Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka watendaji wa ofisi yake kutangaza mafanikio ya wizara na taasisi zake ili wananchi waweze kutambua fursa zinazo wezeshwa na serikali.

Mhandisi Luhemeja amesema hayo Septemba 7, 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili shughuli na kazi za Wizara na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo, kilichofanyika jijini Dodoma.

Amesema ni muhimu kutumia vyombo vya habari kuzungumzia namna ofisi hiyo inavyo ratibu, kusimamia na kukuza sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ustawi wa Watu Wenye Ulemavu.

Aidha ameshauri pia ziandaliwe programu maalum kupitia vipindi vya elimu kwa umma vitakavyo elimisha wananchi kuhusu fursa pamoja na majukumu mengine muhimu yanayotekelezwa na serikali kupitia ofisi hiyo.

Kwa upande wake Mchoraji katuni na Mdau wa Vijana, Ali Masoud (Kipanya) amesema yupo tayari kushirikiana na ofisi hiyo kutangaza mafanikio yanayofanywa na serikali katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na Watendaji Wakuu wa ofisi yake pamoja na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakati wa kikao kazi kilichofanyika Septemba 7, 2023, katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.


Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na Taasisi zake wakisikiliza kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja (hayupo pichani).

Mchoraji katuni na Mdau wa Vijana Ali Masoud (Kipanya) akieleza jambo kuhusu masuala ya maendeleo ya vijana wakati wa kikao kazi hicho.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya ofisi yake wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao kazi hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...