EWURA imevifungia vituo vingine viwili vya mafuta kwa kosa la kuhodhi mafuta, kati ya mwezi Julai na Agosti 2023, Vituo hivyo ni Rashal Petroleum Ltd-Mlimba, Mkoa wa Morogoro na Kimashuku Investment Co. Ltd-Babati, Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Septemba 30/2023, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA  Bw. Titus Kaguo amesema: “Kila tunapokifungia kituo kwa miezi sita tunataka umma ufahamu kwa sababu hawa ndio wanaochangia kusuasua kwa usambazaji wa mafuta hapa nchini.”

Aidha, Bw. Kaguo alisema pamoja na mafuta kuwepo nchini, changamoto ya upungufu wa mafuta katika maeneo mbalimbali ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi ya kibiashara, ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko  la bei za mafuta kinyume na sheria.

EWURA imetoa onyo kali kwa wauzaji wa Jumla na wamiliki wa vituo vya mafuta kuwa Serikali inafuatilia suala hilo kwa karibu kupitia  vyombo vyake mbalimbali  na ikithibitika uvunjaji  wa sheria na kanuni  umetendeka , hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwafutia leseni zao za biashara.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...