WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kama Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya ziara na kusilikiliza kero za wananchi, haoni ni kwa nini watumishi wengine wa umma wanashindwa kufanya hivyo.
 
“Iwapo Mkuu wa nchi, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anaenda kote nchini na kusikiliza wananchi, je ninyi ni akina nani? Nilishasema mtenge siku tatu katika wiki mwende vijijini na kuwasikiliza wananchi,” alisema.
 
Ameyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Septemba 21, 2023) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nguruka, wilayani humo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini, kwenye ukumbi wa NSSF mkoani Kigoma Septemba 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...