Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa siku tatu kwa mamlaka ya maji mijini na vijijini (Ruwasa) wilayani Ludewa kuhakikisha wanaunganisha maji kwenye mradi ulioanzishwa na wananchi katika kijiji cha Luvuyo ambao  ulisimama ili kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa Igongwi ambao unapeleka maji katika halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe.

Agizo hilo amelitoa kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijijj cha Ruvuyo uliofanyika katika kata ya Madope wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Mtaka amesema kijiji cha Luvuyo tayari kina maji ya kutosha hivyo kabla maji hayo kupelekwa sehemu nyingine mamlaka hiyo inatakiwa kuhakikisha maji yanapatikana kijijini hapo ndani ya siku tatu kuanzia sasa.

"Kwasababu maji ya hapa hayahitaji miujiza kwakuwa yapo kwa wakati wote simamisha unapopeleka maji yaanze kuja kwao ili wananchi waanze kutumia maji hayo" alisema Mtaka.

Amesema serikali haiwezi kupuuza hisia za wananchi wa kijiji hicho kuhusu changamoto ya maji wakati uwezekano wa kupata maji upo kwakuwa wana vyanzo vya maji vya uhakika.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa Jeremiah Maduhu alisema kijiji cha Luvuyo kina mradi wa zamani wa maji ambao ulijengwa chini ya ufadhili wa kanisa katoliki mwaka 2012.

Amesema chanzo cha maji katika mradi  huo kumejengwa mradi mwingine wa maji wa Igongwi ambapo taharuki kwa wananchi wa kijijj hicho imekuja wakidhani huenda maji hayo yanahamishwa kupelekwa eneo lingine wakati wao hawana maji kijijini hapo.

"Baada ya kuwa changamoto imeonekana maji yakitoka kwenye chanzo ambacho kimejengwa kwa ajili ya mradi wa maji wa Igongwi kwenda Njombe chanzo cha maji ambacho  kinahudumia hapa Luvuyo maji yalikuwa hayawezi kufika kwa wananchi hivyo kusababisha changamoto ya upatikanaji wa maji" alisema Maduhu.

Nao wananchi wa Kijiji cha Luvuyo kilichopo kata ya Madope wilayani Ludewa mkoani Njombe waliishukuru serikali kwa kuingilia kati changamoto ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ambayo ilikuwa inawasumbua kwa muda mrefu.

Wamesema walichanga fedha kwa viboko na kuwekwa mahabusu ili mradi huo wa maji uweze kukamilika lakini wameshangaa kuona serikali inajenga chanzo kingine cha maji juu ya kile cha awali na kusababisha wao kukosa maji kabisa.

Mmoja ya wananchi wa kijijj cha Luvuyo Matrida Mgimba alisema changamoto ya maji kijijini hapo inawaathiri hata wanafunzi wa shule kwani wanalazimika kukosa masomo kutokana na kufuata maji mtoni wakati huo vipindi vinaendelea darasani.

"Wanafunzi wananyanyasika sana kuchota maji mtoni muda wa vipindi unafika maji hayatoshi inabidi wachaguliwe wengine wachote maji hivyo wanakosa masomo na kusababisha kuathirika kitaaluma" alisema Mgimba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...