Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali Mapingamizi yaliyowekwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa mke wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake akitaka upande wa Jamuhuri usikubaliwe maombi yao ya kutaka kumleta shahidi aliyekwisha kutoa ushahidi, kumuongeza shahidi aliyekuwa mtunza vielelezo na na kutoa taarifa ya awali (first crime Report) kwa sababu Mapingamizi yao hayana mashiko.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 6, 2023 na Jaji Edwin Kakolaki anayesikiliza kesi hiyo.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 ni wifi wa marehemu, Aneth, mjane wa Bilionea Msuya; Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella.

Aneth alifariki dunia Kwa kuchinjwa shingoni Mei 25, 2016, usiku nyumbani kwake, Kibada Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo).

Akisoma uamuzi huo, Jaji Kakolaki amesema amepitia kwa kina hoja zilizotolewa na pande zote mbili na pia baada ya kupitia kumbukumbu za mahakama hakuna ubishi kuwa nakala ya taarifa ya awali ( first crime Report) ilitolewa na kupokelewa kama kielelezo D3 na shahidi wa nne wa upande wa Jamuhuri Sajenti Obadia ambaye alikataa kufahamu kilichomo ndani ya kielelezo hicho na pia hakuulizwa lolote.

Shahidi huyo, Inspekta Obadia alipoitwa mahakamani hapo hakuulizwa swali lolote la dodoso kujua walichokuwa wanakitafuta upande wa utetezi mpaka.alipoitwa shahidi wa 22, SSP Mhanaya na kuulizwa maswali ya dodoso.

"Nakubaliana upande wa Jamuhuri kuwa kifungu cha 147 (4) hakikatazi kuita tena shahidi. Lakini pia Mahakama inaona kuwa upande wa utetezi utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali ili kujua walichotaka kukifahamu katika taarifa hiyo . Hivyo pingamizi hili linakataliwa

Akijibu kuhusu pingamizi la kuongeza shahidi, Jaji Kakolaki amesema, hakuna ubishi taarifa hiyo iko katika maandishi imekidhi kigezo cha kwanza na kuna majina ya shahidi, kielelezo kitakacholetwa na maelezo ya ushahidi unaotakiwa kuletwa kama kifungu cha 289(4) CPA kinavyoeleza na hivyo mahakama imechunguza notisi hii na kuona imetimiza matakwa yote ya kisheria.

Amesema, maelezo yaliyotolewa ambayo ni taarifa halisi ya awali ya tukio la uhalifu iliyotolewa Kwa RCO Temeke na kwa DCI.

Kuhusu maelezo ya shahidi Obadia Jaji Kakolaki ameeleza kuwa yeye ndiye aliyepokea taarifa hiyo na ndio mtunza nyaraka na kumbukumbu ofisi ya DCI.

Hata hivyo, Jaji Kakolaki ameiagiza upande wa mashtaka wawapatie upande wa utetezi nakala hiyo ya taarifa ya awali kufikia Septemba 2023 na wasipofanya hivyo hawataruhusiwa kutumia ushahidi huĆ³

Kuhusu hoja ya notisi kutokusainiwa mahakama imeona halina mashiko kwa kuwa Mahakama unaongozwa na nyaraka iliyowasilishwa mahakamani ambayo imekidhi matakwa ya kisheria.

Kuhusu kuahirishwa kwa minajili ya haki ni bora Mahakama hii ikaruhusu ahirisho Ili kuwapa nafasi ya kuandaa na kuleta mashahidi hivyo kwa kesho haitawezekana.

Mapema wakili wa serikali Mwandamizi Yasinta Peter aliwasilisha mahakamani hapo ombi la kumuita upya shahidi wa nane katika kesi hiyo ili aje afafanue juu ya kilelelezo cha First crime Report kwa sababu ushahidi juu ya kielelezo hicho ulitolewa mahakamani na kurekodiwa.

Amesema shahidi huyo, mstaafu wa jeshi la polisi Inspekta Fredrick Nyudike ndio aliandaa first crime Report lakini kwenye ushahidi wake hakuongelea hiyo ripoti wala hakufanyiwa cross examination (dodoso) ingawa ripoti hiyo imetumika katika kumuuliza maswali ya dodoso SSP David Mhanaya.

Aidha Yasinta aliiomba mahakama kumuondoa kwenye orodha ya mashahidi shahidi namba 23, Inspekta Jumanne ambaye alipaswa kutoa ushahidi wake leo Septemba 6,2023 mahakamani hapo wa kuwa ushahidi wake unafanana na ushahidi wa shahidi aliyekwisha maliza kutoa ushahidi wake.

"Mheshimiwa leo tulitarajia kuwa na shahidi SSP Inspekta Jumanne Malangahe lakini tumegundua kuwa ushahidi wake unafanana wa Jamuhuri ambaye amekwisha toa ushahidi hivyo upande wa Jamuhuri tunaomba kumuondoa". Amesema Yasinta.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala amepinga ombi hilo la kumuita upya shahidi wa nane akidai kuwa shahidi huyo teyari alifika mahakamani na kutoa ushahidi wake huku akiwa na first crime Report.

Kibatala amedai kuwa, hiyo ripoti ilitolewa Mahakamani hapo na shahidi wa Jamuhuri sasa kuna ulazima gani wa kumuita tena shahidi wa nane ambaye amekwisha toa ushaidi wake zaidi ya miezi nane iliyopita.

"Mheshimiwa Jaji, ombi la kumuita tena shahidi huyo linatokana na cross examination (Dodoso) niliyofanya kwa Mhanaya wanataka kuja kuziba mapengo, kama watakuwa wanawaita upya mashahidi wao baada ya sisi kufanya Cross (kuuliza maswali ya dodoso) basi kesi zitakuwa haziishi.

Amedai kuwa toka kuanza kwa vikao vya kesi hii (session) vile vya mwezi Juni na sasa upande wa Jamuhuri wameshaleta notisi kadhaa, Mwanzo waliomba kumongeza daktari aliyefanyia uchunguzi wa mwili wa marehemu na leo tena wanaomba kurudia kumuita shahidi na kuongeza nyaraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...