Na Muhidin Amri Tunduru

ZAHANATI ya kijiji cha Njenga kata ya Mchoteka Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,imepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kwa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi vitakavyosaidia  utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Vifaa vilivyotolewa na kanisa hilo ni vitanda  vya kulala  watu wazima,vitanda vya kujifungulia vitanda kwa watoto wadogo na viti vya magurudumu manne(wheel chairs) kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa mtu mwingine ili kuwafikia watoa huduma.

Akipokea vifaa hivyo,muuguzi wa zahanati ya Njema Upendo Bora,amelishukuru Kanisa hilo kwa msaada huo kwani vifaa hivyo vitakwenda kuchochea uwajibikaji kwa watumishi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma za afya.

Alisema,vifaa hivyo vimetolewa kwa muda muafaka kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaofika katika kijiji hicho  kwa ajili ya shughuli mbalimbali wakiwemo wanunuzi wa mazao na wafugaji ambao watahitaji  kupata matibabu.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Njenga John Mtanga alisema,msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na kanisa hilo vitapunguza kero ya mama wajawazito wanaosubiri kujifungua au waliojifungua kulala zaidi ya mtu mmoja katika kitanda kimoja.


Mtanga,amewaomba wadau na watu wenye uwezo kuisaidia zahanati hiyo ambayo inauhitaji mkubwa wa vifaa tiba,watumishi na dawa ili kuokoa maisha ya watu na kupunguza muda wa wagonjwa kwenda maeneo mengine kufuata huduma za afya.


Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Noel Mbawala alisema,kanisa kupitia taasisi yake ya Kiuma imelazimika kutoa vifaa hivyo ili vitumike kuimarisha afya za watu kwa kutambua kuwa ili watu waweze kumjua Mungu na kushiri kwenye shughuli za maendeleo ni lazima wawe na afya njema.


Aidha alisema,kanisa limetoa vifaa tiba katika zahanati hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya vifaa kwa ajili ya wagonjwa na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita za kuimarisha na kuboresha huduma za afya katika wilaya ya Tunduru.


Alisema,kanisa la Upendo wa Kristo Masihi litaendelea kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo kwa kutambua kuwa,serikali haiwezi kufanya kila kitu pekee yake, hivyo zinahitaji nguvu za pamoja ili kufanikisha mipango yake.


Askofu Mbawala,ameipongeza serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jithada zake katika kuimarisha huduma za afya,maji,umeme na miundombinu ya Barabara ambayo imewezesha kuboresha na kuimarisha maisha ya Watanzania.
MWISHO.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Njema kilichopo mpakani mwa wilaya ya Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma,wakifurahi baada ya zahanati ya kijiji hicho kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi-Kiuma ili viweze kuboresha huduma bora  katika zahanati hiyo,katikati Askofu mkuu wa Kanisa hilo Noel Mbawala
Muuguzi wa zahanati ya kijiji cha Njenga wilayani Tunduru Upendo Bora kulia na mwenyekiti wa kijiji  hicho  John Mtanga  katikati,wakipokea moja ya vitanda vya kulaza wagonjwa kutoka kwa Askofu wa kanisa la Upendo wa Kristo Masihi lililopo kijiji cha Milonde wilayani Tunduru Noel Mbawala,kwa ajili ya kulaza wagonjwa watakaofika kupata huduma  za afya.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Noel Mbawala kushoto,akikabidhi kiti cha madurudumu mawili kwa muuguzi wa zahanati ya Njenga wilayani Tunduru Upendo Bora kulia, kwa ajili  ya wagonjwa watakaofika kupata huduma za matibabu katika zahanati hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...