Na Rahma Khamis Maelezo              16/9/2023

 

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe, Tabia Maulid Mwita ameitaka Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kuweka sheria ndogondogo zitakazowabana wanaochafua fukwe za bahari ili kutunza mazingira nchini.

 

Wito huo ameutoa wakati akizundua na kushiriki zoezi la usafi katika Fukwe za Maruhubi Wilaya ya Mjini ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Usafi Dunani.

 

Amesema usafi wa mazingira hasa katika fukwe za bahari ni njia moja wapo ya kuvutia Watalii kufika Zanzibar hivyo kuwepo kwa sheria hizo zitasaidia kuongeza pato la Tafa linalotokana na wageni hao.

 

Aidha amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kusimamia na kuhakikisha suala la usafi linaimarika katika maeneo yote ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafu.

 

Waziri Tabia  amefahamisha kuwa taka ni ajira kwa wananchi  hivyo ni wajibu wa Taasisi husika   kuhakikisha taka hizo  zinatunzwa na kuhifadhiwa katika sehemu salama ili kuepusha uchafuzi wa mazingra.

 

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu na kutoa elimu kwa watumiaji wa fukwe juu ya umuhimu wa kutunza fukwe ili kuepusha madharayanayoweza kujitokeza.

 

Hata hivyo Waziri amewashukuru  Wadau waliochangia   vifaa vya usafi jambo ambalo litasaidia kuimarisha huduma za usafi  na kuwataka wananchi kushirikiana katika kuhimizana suala la usafi kwa vile Zanzibar ni kitovu cha utalii.

 

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Fatma Mbarouk amesema wageni wengi bado hawaridhishwi  na hali ya usafi wa Mji hasa katika fukwe  hivyo amewataka wadau wa usafi kuongeza  jitihada kuhakikisha hali hiyo inaondoka.

 

Nao wananchi wa maeneo hayo wamesema usafi ni swala la msingi katika jamii hivyo kila  mmoja ana haki ya kutekeleza wajibu wake kwa kuimarisha katika eneo  lililomzunguka.

 

Aidha  wamefahamisha kuwa  sehemu ambayo haina usafi maradhi hayakosekani hivyo wamewaomba wananchi wenzao kushiriki katika suala la  usafi ili kujikinga na  madhara yanayoweza kuepukika.

Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Fatma Mbarouk Khamis akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita kuzindua zoezi la usafi katika maadhimisho ya siku ya usafi Duniani, hafla iliyofanyika Fukwe za Maruhubi Mjini Unguja.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati akizindua zoezi la usafi katika maadhimisho ya siku ya usafi Duniani huko  Fukwe za Maruhubi Mjini Unguja.
Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa akizungumza na Waandishi wa Habari  juu ya umuhimu wa usafi wa Mji katika maadhimsho ya siku ya usafi Duniani yaliyofanyika Fukwe za Maruhubi Mjini Unguja.


PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...