*Asema kama kuheshimu vitabu vya dini hata Katiba hutaieshimu


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Katiba sio mali ya Wanasiasa bali ni ya Watanzania wote na kwamba ili kuufanikisha Katiba lazima elimu itolewe ili kila mmoja awe na ufahamu.

Akizungumza leo Septemba 11, 2023 jijini Dar es Salaam na Baraza la Vyama vya Siasa, Rais Samia ametumia nafasi hiyo kuzumgumzia mchakato wa Katiba mpya ambapo amesema yametolewa maoni mengi.

"Maoni yamekuja kila upande wale waliotaka peke yao Katiba, kikosi cha siasa kikubwa Katiba, Zanzibar wote wamesema Katiba , na wote tulitoa kauli kwamba tumekubaliana na tunakwenda na marekebisho ya Katiba yetu.Tumekubaliana.

"Lakini jambo hili ni mchakato na kwa bahati nzuri Katiba si mali ya wanasiasa, si mali ya vyama vya siasa ni ya watanzania awe ana chama , awe hana chama , awe ana dini awe hana.

"Awe mrefu awe mfupi , mnene mwembamba, mkubwa aumdogo, Katiba ni ya watanzania.Kwa hiyo matengenezo yake yanahitaji tafakuri na kubwa sana hatuwezi kuchipuka tu pwaaa haya.

"Unachukua Katiba ya Warioba inasemaje, Katiba ya Kenye inasema, kifungu kinasemaje , hatuendi hivyo hii ni mali ya watanzania.Tunataka tukifanya marekebisho ituchukue muda kitabu chetu kiende...

" Lakini Katiba ni kitabu tunaweza kutengeneza kitabu kizuri, tukakipamba , tukakiweka, wangapi wanakielewa hicho kitabu? Yaliyomo humo ndani wangapi wanaelewa, Katiba tuliyonayo wanaielewa ?

"Unakwendaje kumuuliza mtanzania nipe maoni yako wakati kitu haikijui, tunaanza na elimu ya watanzania wajue ni kitu gani , wajue kinasemaje, kina nini lakini tunakwenda viongozi wa kisiasa huku tukidhani tuna haki ya kuburuza watu tunachokisema sisi watu wote waseme hivyo." amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa wamewageuza watu makasuku."Tnataka Katiba mpya, watu waseme , mtu ukimuuliza kifungu gani kinauzi hakuna!hajui ! au unataka nini kibadilike maana ndio tunataka mpya, tunataka mpya tu

"Sasa mpya ilete nini ?Unajua ndio hivyo ndio maendeleo, nani kasema maendeleo yanaletwa na kitabu kilichotungwa kikawekwa pale? Kama kuheshimu vitabu tungeheshimu vya dini sio ndio vya kuheshimiwa?

"Wangapi tunaviuka hatuvishemu , na huwezi kuheshimu kitabu mpaka ujue maana yake, hata cha dini huwezi kuheshimu Masihafu yako, Biblia yako kama hujui humo ndani kuna nini ...

" Na ndio maaa unaona kuna wengine wanachukua wanalala nayo lakini matendo tofauti, hayaendani. Tunakwenda tunadhani tuna haki kuburuza watu tunachokisema sisi watu wote wakifuate tunageuza watu makasuku."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...