*Awaambia hakuna aliyejuu ya shria, ukikosea itakushika

*Awajia juu watoa lugha chafu kama hawakulelewa na wazazi wao

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan Tanzania amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa nchini kuwa hakuna aliyejuu ya sheria na kila atakafanya kosa sheria itamshika.

Akizungumza leo Septemba 11, 2023 katika kikao kati yake na Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Rais Samia amewakumbusha viongozi wa vyama vya suasa na wanasiasa kuhusu kuheshimu sheria za nchi.

“Kuna sifa za peke yetu ambazo wazee wetu walizisuka, wakazijenga na kutumbia hivi ndio jinsi ya kwenda, hivyo yoyote anayeitakia mema nchi hii atakwenda kwenye misingi hiyo wala hata kopi misingi ya watu huko yanakotoka , ailete hapa…

“Halafu atake tuitekeleze, hapana tuna mila na desturi ya mambo yetu ya kitanzania tutakwenda kwa misingi hiyo.Hakuna aliyejuu ya sheria, hakuna, hakuna, hakuna.

“Kila anayefanya makosa sheria itamshika, kama umekiuka sheria itakushika.Kwa hiyo hiyo tutambue hakuna aliyejuu ya sheria na ajenda yetu kubwa kama watanzania ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa,”amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa mambo hayo ndio wamekuwa wakiyafanya miaka yote na hadi sasa wanachofanya ni hicho hicho ,hivyo kama jukwaa la vyama vya siasa madhumuni yake ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa

Rais Samia amesema kila mtu kwa kila mahala ambapo Mungu amemjaalia kumuweka kwa ajili ya kujenga taifa letu, kama ni mkulima alime au mvuvi kila mmoja kwa upande wake.

“Sasa kama kuna wengine wana roho za kutu kuona tu Tanzania iko kwenye mgogoro hao sio wenzetu.Hao sio wenzetu na sio madhumuni ya kuruhusu mikutano, kwa hiyo kuna uhuru wa maoni lakini uhuru wa maoni unamipaka yake sio tu kisheria hata kibinadamu

“Kama ulizaliwa na ukalelewa vema , ukapitishwa kwenye masomo ya kawaida na masomo ya dini na ukailewa dini yako vizuri kuna mambo huwezi kufanya tu.

“Huwezi kusimama ukafanya mambo ambayo kama mwendawezi raha yake aone ugomvi, mabishano na huyu uamue leo useme unampa Serikali leo na wenzake kama kikundi ataunda chama kingine awapinge wale wale wenzie aliokuwa nao.”

Akieleza zaidi Rais Samia amesema na ndio wanayowaona huko kwao ukiona hawako hapa sio tu kwamba labda kuna kununa lakini hakukaliki huko ndani, kuna moto wengine waende wengine wasiende, kuna moto huko.

Amesema sasa tabia kama hizo watakuwa na amani kweli , hawawezi kuwa na amani.“Kwa hiyo ndugu zangu uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake…

“Kama ulizaliwa na baba yako na mama yako ukalelewa vema ukapitishwa kwenye misingi ya dini maneno mengine huwezi kusema.

“Mengine tunayoshuhudia huko kwenye mitandao mtu aliyeyelewa vizuri hawezi kusema .Sasa sio wote tumepata bahati hiyo ya kulelewa ukapitishwa vizuri ukakua ukajua dunia inaendaje sio wote,”amesema Rais Samia.

Amesisitiza wangine wamechipuka tu, wameona dunia ndio hii hapa kama kipofu kaona jua halafu kaona jogoo .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...