* Ataka huduma bora kuwafikia wananchi

Na Mwandishi Wetu Dodoma,

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka watendaji wa ofisi yake kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa malengo yanayopimika ili kuiwezesha serikali kufikia malengo na kuwahudumia wananchi.

Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo Septemba 5, 2023 mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Prof. Jamal Katundu ambae amehamishiwa Wizara ya Maji.

Ameongeza kuwa, kazi ya kuhudumia wananchi haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu kwa maslahi mapana ya taifa.

Aidha, ameahidi kushirikiana na menejimenti na watumishi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ofisi hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Jamal Katundu ameishukuru Menenjimenti na Watumishi kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ambao ulimwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akikabidhiwa nyaraka kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza menejimenti ya ofisi hiyo baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, hafla iliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha makabidhiano kilichofanyika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu akieleza jambo mara baada ya makabidhiano ya ofisi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa sita kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu (wa sita kutoka kulia), wakiwa katika picha ya Pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyobaada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Wizarani hapo, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

 

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...